SHULE YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA VYOO
Diwani
wa kata ya Mgama Denis Lupala akizungumza na wanafunzi wa shule ya
sekondari ya Mgama wakati alipowatembelea na kula pamoja chakula cha
mchana.
Diwani wa kata ya Mgama Denis Lupala akizungumza na mwalimu mkuu wa shule hiyo Simeone Lihuluku.
Diwani
wa kata ya Mgama, Denis Lupala akimpakulia chakula mmoja wa wanafunzi
wa shule ya sekondari ya Mgama wakati alipowatembelea na kula pamoja
chakula cha mchana
baadhi
ya wanafunzi shule ya sekondari ya Mgama wakiwa katika foleni ya
chakula kilichoandaliwa na diwani wa kata ya Mgama Denis Lupala.
Na Denis Mlowe,Iringa
SHULE
ya sekondari Mgama iliyoko katika kata ya Mgama jimbo la Kalenga wilaya
ya Iringa Vijijini inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa matundu ya
vyoo 30 yaliyopo 12 na miundo mbinu mibovu.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi wakati wa hafla iliyoandaliwa na diwani wa
kata hiyo Denis Lupala,Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Simeone Lihuluku
alisema kuwa licha ya upungufu wa matundu ya choo shule hiyo inakabiliwa
na ukosefu wa maktaba na maabara kwa wanafunzi wanaosoma shuleni hapo
tangu kuanzishwa kwake miaka saba iliyopita.
Luhuluku
alisema shule hiyo inakabiliwa na ukosefu wa mabweni ya wanafunzi na
nyumba za kuishi walimu kitu kinachochangia wanafunzi kupanga mbali na
maeneo ya shule changamoto inayosababisha ufaulu hafifu kutokana na
utoro pamoja na upatikanaji wa mimba kwa watoto wa kike.
Alisema
mwaka huu tayari wanafunzi watatu wamekatisha masomo kutokana na kupata
ujauzito huku nyumba za walimu zinazohitajika zikiwa 18 na zilizopo kwa
sasa ni nyumba mbili za walimu.
“Licha
ya upungufu wa matundu ya vyoo vilevile tunakabiliwa na changamoto
nyingi sana katika shule hii lakini kubwa zaidi ni ukosefu wa maabara na
maktaba kwa ajili ya wanafunzi na tumekuwa tunatumia chumba kimoja cha
darasa kama maabara kitu kinachosabisha wanafunzi kutosoma vizuri na
kupunguza ufaulu naomba sana wadau waweze kuwasaidia kuondokana na
changamoto hizi” alisema Lihuluku
Aliongeza
kuwa shule hiyo imekosa huduma ya umeme,vyanzo vya kuaminika vya maji
safi na vifaa vya kufundishia pamoja na uchangiaji hafifu wa michango ya
shule kwa wazazi.
Kwa
upande wao wanafunzi wa shule hiyo wamemshukuru diwani huyo kwa
kuwaandalia chakula huku wakimuomba kuwasaidia kutatua changamoto
zinazowakabili katika shule yao kwa lengo la kuongeza ufaulu shuleni
hapo.
Shule
ilianzishwa mwaka 2007 ikiwa inatoa elimu ya kidato cha kwanza hadi cha
nne ikiwa na jumla ya wanafunzi 516 kati ya hao wavulana wakiwa 221 na
wasichana 295 na walimu 20.
SHULE YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA VYOO
Reviewed by crispaseve
on
23:23
Rating:

Post a Comment