Wanariadha waahidi kuleta heshima katika mashindano ya Jumuiya ya Madola nchini Sctoland
Kocha wa
wachezaji wa Riadha waliokuwa nchini Ethiopia kwa ajili ya maandalizi ya
mashindano ya Olympic yanayotarajia kufanyika kuanzia 23, Julai, 2014 jijini
Glasgow Scotland Bw. Shaban Hiiki (mwenye suti nyeusi) akiwa na baadhi ya
wanamichezo hao mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
Kocha wa wachezaji wa Riadha waliokuwa
nchini Ethiopia kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Olympic yanayotarajia
kufanyika kuanzia 23, Julai, 2014 jijini Glasgow Scotland Bw. Shaban Hiiki
(mwenye suti nyeusi) akiwa na baadhi ya wadau wa mchezo wa Riadha waliojitokeza
kuwapokea wachezaji wa mchezo huo mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
Kocha wa wachezaji wa Riadha
waliokuwa nchini Ethiopia kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Olympic
yanayotarajia kufanyika kuanzia 23, Julai, 2014 jijini Glasgow Scotland Bw.
Shaban Hiiki (mwenye suti nyeusi) akiwa na baadhi ya wanamichezo hao mara baada
ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere
jijini Dar es Salaam jana.Picha na Frank Shija, WHVUM
Na Frank Shija, WHVUM
Wanamichezo waahidi kuleta medali katika
mashindano ya Olympic yanayotarajia kuanza tarehe 23 Julai jijini Glasgow Scotland.
Akizungumza mara baada ya kuwasili nchini
jana wakitokea Ethiopia Kocha wa Timu ya Riadha aliyeambatana na wachezaji 8
Bw. Shaban Hiiti alisema kuwa ana imani kubwa na wachezaji wake walioteuliwa
katika Timu ya Taifa kuwa watailetea heshima Taifa kwa kuwa mazoezi
waliyoyapata wakiwa nchini Ethiopia yamewajengea uwezo mkubwa.
Hiiki aliongeza kuwa walipokuwa nchi
Ethiopia kwa mazoezi wamejifunza mbinu mbalimbali kutokana na kuwa na program
za kuwajengea uwezo wachezaji wake. “Nimatumaini yangu wachezaji hawa
walioteuliwa kujiunga na wenzao waliokuwa mazoezini katika nchini zingine
ambapo wanamichezo wetu walienda kwa ajili ya mazoezi wataliletea Taifa letu
heshima kubwa kwani wamepikwa wakapikika”. Alisema Kocha huyo.
Aidha kocha huyo amesema kuwa uwepo
mazingira mazuri na vifaa bora vya mazoezi kumechangia kwa kiasi kikubwa kuinua
ubora wa wanariadha hao ambao wamefanya mazoezi kwa takribani miezi miwili
nchini Ethiopia. Kwa upande wake mmoja wa wanariadha ambaye
amebahatika kuitwa kwenye kikosi kitakachoshiriki mashindano hayo Bw. Alphonce Felix
amesema kuwa anajisikia faraja kuwa miongoni mwa wanamichezo watakao iwakilisha
nchi katika mashindano ya Olympic kupitia mchezo wa riadha.
Alphonce amesema kuwa atatumia ujuzi
alioupata nchini Ethiopia walipokuwa wameweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya
mashindano hayo. Jumla ya wanariadha 9 na kocha wao waliweka
kambi nchini Ethiopia ikiwa ni jitihada zinazofanywa na Serikali za kukuza na
kuendeleza Sekta ya Michezo nchini kupitia mpango wa Diplomasia ya Michezo,
ambapo wanamichezo mbalimbali wameweka kambi ambao wanamichezo wengine waliweka
kambi katika nchi za Uturuki, China na New Zealand.
Wanariadha waahidi kuleta heshima katika mashindano ya Jumuiya ya Madola nchini Sctoland
Reviewed by crispaseve
on
05:34
Rating:
Post a Comment