Anglikana laridhia wanawake maaskofu

Kanisa kuu la Anglikana Uingereza
Baraza kuu la kanisa la Kianglikana Uingereza, The General Synod, limeidhinisha wanawake kuwa maaskofu.
Maafisa katika kanisa hilo wanaamini wana ufuasi mkubwa unaounga mkono hoja hiyo.
Sasa baada ya kupitishwa kwa kura hiyo, huenda askofu wa kwanza mwanamke akachaguliwa kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
Makasisi
wanawake walio thuluthi moja ya viongozi wa kidini wa kanisa la
kianglikana, wanasema haki sawa itawapandisha hadhi katika makanisa.
Hatua
hiyo inemaliza mvutano wa miaka mingi na kuvunja utamaduni wa makarne
katika kanisa hilo. Tofauti nyingi zimeibuka kuhusu suala hilo na hata
kusababisha migawanyiko katika kanisa hilo ambapo baadhi ya ma dayosisi
yameshawatawaza maaskofu wanawake, na kukaidi amri la hapo awali la
kanisa kuu.
Nchi zilizo na maaskofu wanawake:New Zealand,Australia,Marekani,Canada na Afrika Kusini
'Msimamo wa viongozi wa kanisa hilo Afrika'

Kasisi
Moses Bushendich kutoka kanisa la Kianglikana Uganda ameambia BBC kuwa
misimamo imegawanyika juu ya maaskofu wanawake kutokana na mafundisho ya
Bibilia.
''Kanisa
la Afrika halina uamuzi wa pamoja juu ya suala hili. Kila tawi
limechukua msimamo wake baadhi wanapinga na wengine wanaunga mkono''
amesema kasisi Bushendich.
Baadhi
ya itikadi ambazo zimekuwepo kwa miaka m ingi katika makanisa kuu kama
vile Katoliki na Anglikana ni wanawake kuwa maaskofu wanawake, na
kruhusu ndoa ya wapenzi wa Jinsia moja ambayo tayari baadhi ya maumini
na maaskofu wa kanisa hilo wamepigia debe kuidhinishwa.Chanzo BBC
Swahili
Anglikana laridhia wanawake maaskofu
Reviewed by crispaseve
on
06:33
Rating:
Post a Comment