Benki ya Exim yazindua mafunzo maalum kuongeza tija kwa wafanyakazi
Mkuu wa kitengo cha Oparesheni wa Benki
ya Exim Tanzania, Eugen Massawe (wapili kushoto) akikata utepe kuzindua mafunzo
maalum kwa wafanyakazi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja
Mwandamizi wa Mafunzo na Maendeleo wa kituo cha mafunzo cha Exim Academy, Bi
Priti Punatar na Kushoto ni Beatus Temba, mkufunzi katika kituo hicho.
Meneja Mafunzo na Maendeleo wa Exim
Academy, Japheth Oyugi akiwafunza baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Exim
Tanzania wanaopata mafunzo hayo mara baada ya uzinduzi wa mafunzo maalum
yatakayotolewa na kituo hicho cha mafunzo jijini Dar es Salaam jana.
Benki ya Exim Tanzania imezindua
mafunzo maalum, yakiwa na lengo la kuwapatia maafisa wake wapya na wa zamani wa
matawi mbali mbali wa benki hiyo ujuzi katika shughuli a kibenki za kimihamala
na juu ya sera za udhibiti ili kuimarisha tija kwa wafanyakazi na kuboresha
utoaji wa huduma kwa wateja.
Mafunzo hayo yatakuwa yakitolewa kwa
wastani wa, masaa 56 ya mafunzo kwa maafisa mpya wa matawi mbali mbali ya
benki, pamoja na masaa 160 kwa mafunzo yatakayokuwa yakiendelea ya darasani kwa
maafisa wote wa matawi ya benki hiyo, kila mwaka.
Akizungumza wakati wa sherehe za
uzinduzi wa mafunzo hayo uliofanyika katika kituo cha mafunzo ya benki ya Exim
cha 'Exim Academy' jijini Dar es Salaam jana, Meneja Mwandamizi wa Mafunzo na
Maendeleo wa Benki ya Exim, Bi Priti Punatar alisema mafunzo hayo yanalenga
katika kuboresha shughuli za matawi katika mazingira yaliyo salama na kupima
ujuzi wa utatuaji wa matatizo mbali mbali bila kuwepo kwa viashirio vya majanga
ambayo taasisi za kifedha ukumbana nayo katika dunia halisi ya masuala ya
kibenki.
"Leo tunazindua mafunzo maalum
ambayo yatawapatia maafisa wetu wa benki katika matawi mbali mbali ujuzi katika
shughuli za kibenki za kimihamala na juu ya sera za udhibiti.
"Wafanyakazi wetu watapewa mafunzo
juu ya majukumu mbalimbali katika tawi ili kuwajengea uelewa zaidi juu shughuli
za kibenki na kuboresha za ujuzi wao katika biashara za masuala ya kibenki.
Tunatarajia kuwa njia hii mpya itasaidia kuon geza ufanisi wetu katika shughuli
zetu na kutuwezesha kufikia lengo la kufikia matakwa ya mteja, "alisema.
"Mafunzo haya yataongeza ufanisi
kwa wafanyakazi wetu na tija, na hivyo kuboresha utoaji wa huduma kwa
wateja," alisema Bw Eugene Masawe, Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji
katika Benki.
Alibainisha kuwa, mafunzo hayo
yatawawezesha wafanyakazi kujifunza kwa vitendo, mbinu za kuthibitika
zitumikazo katika sekta kwa kutumia vifaa vya kipekee, ikiwa pia inalenga
katika kuboresha na kurahisisha taratibu mbali mbali za kibenki katika benki.
"Tumeanzisha mafunzo haya tukiwa
na lengo si tu
kuongeza jitihada za kufikia matakwa ya mteja bali pia kutoa msaada bora wa
huduma kwa wateja wetu wote na kuongeza ufanisi na kupunguza makosa
yanayojitokeza ya kibenki katika shughuli zetu za kila siku.
"Kupitia mafunzo haya, wafanyakazi
wetu pia watakuwa na uwezo wa kutathmini na kukabiliana na majanga
yanayohusiana shughuli za kimihamala za kibenki, kukidhi mahitaji ya udhibiti,
kuhakikisha wafanyakazi wanatumia fursa zote za kimauzo zinazojitokeza, hivyo
kuboresha utoaji huduma kwa wateja," aliongeza Masawe.
Pia alisema kuwa mafunzo hayo
yataiwezesha benki yake kufikia malengo ya kuendeleza wafanyakazi wa benki hiyo
kwa kuwa na ujuzi wa uhakika katika masuala ya kibenki na utoaji wa
huduma.
Exim Academy ni kituo cha mafunzo kilichothibitishwa
kikiwa na cheti cha ISO 9001:2008 kilichoundwa kwa ajili ya wafanyakazi
wa Benki ya Exim ambacho utoa mafunzo tofauti yakiutendaji, uongozi na
utoaji wa huduma bora, na kujenga uhusiano nzuri na mteja kwa ujumla.
Benki ya Exim yazindua mafunzo maalum kuongeza tija kwa wafanyakazi
Reviewed by crispaseve
on
08:10
Rating:

Post a Comment