KITABU CHA "HISTORIA YA KLABU YA SIMBA"KILICHOANDIKWA NA MWINA KADUGUDA CHAZINDULIWA RASMI LEO
Naibu
Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa
Juma Nkamia Akijiandaa kukata utepe ili kuweza kuzindua rasmi kitabu
hicho cha historia ya Simba,Wanaoshuhudia kulia ni mtunzi wa kitabu
hicho Mwina Kaduguda akifuatiwa na Bwana Mkuki Bgoya mkurugenzi wa Mkuki
na Nyota Ambao ndio wachapishaji wa kitabu hicho.
Mwina
Kaduguda Mtunzi wa kitabu cha "HISTORIA YA SIMBA" akielezea kwa kina
Magumu gani amepitia wakati anaanza kuandaa kitabu hicho,Wa kwanza
Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia na Katikati ni Mkurugenzi wa Mkuki na
Nyota Bwana Mkuki Bgoya ambao ndio wachapishaji wa kitabu
hicho.Akielezea kwa ufupi Mwina Kaduguda amesema kwamba Dhumuni kubwa la
Kutunga kitabu hicho ni kutaka kutunza historia ya soka ya Timu hiyo
isipoteee ili iweze kusomwa kizazi na kizazi.
Mkurugenzi wa Mkuki na Nyota Bwana Mkuki Bgoya Akielezea namna walivyochapa kitabu hicho na ubora wake .
Mjumbe
wa kamati ya Utendaji Klabu ya Simba Bwana Collin Frisch akiongea kwa
niaba ya Rais wa Simba,ambapo amempongeza sana Mwina Kaduguda na kusema
ameiweka Klabu ya Simba kwenye Kumbukumbu muhimu sana kwenye soka la
Tanzania hivyo inatakiwa aungwe mkono kwa nguvu zote.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa
Juma Nkamia akitoa neno kumpongeza Mwina Kaduguda kwa kufikiria mbali
sana kwa kuweka soka la Tanzania kwenye maandishi namna klabu ya simba
ilivyoanza,Akaongeza kuwa Klabu za soka Tanzania zinatakiwa kuwa na watu
kama Mwina Kaduguda ili kuleta maendeleo ya soka.Naibu waziri pia
akasisitiza ni wakati wa kila mwanachama kujituma kwa bidii na kuacha
kukaaa kwenye korido za Klabu na kupiga Zoga.
Mwina
kaduguda Mtunzi wa Kitabu cha "HISTORIA YA SIMBA" Akimkabidhi Naibu
Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma
Nkamia Zawadi ya Kitabu ambayo ameomba apelekewe Rais Jakaya Mrisho
Kikwete. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
KITABU CHA "HISTORIA YA KLABU YA SIMBA"KILICHOANDIKWA NA MWINA KADUGUDA CHAZINDULIWA RASMI LEO
Reviewed by crispaseve
on
03:10
Rating:
Post a Comment