KOMWETA HEMED MANETI A.K.A CHIRIKU WA VIJANA JAZZ AFUATA NYAYO ZA MAREHEMU BABA YAKE HEMEDI MANETI ULAYA
Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku mwanamuziki wa bendiya Vijana Jazz
Marehemu Hemedi Maneti Ulaya Chiriku aliyekuwa mwamuziki wa bendi ya Vjana Jazz enzi hizo.
......................................................................................................
Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku ni Mtoto wa mwanamuziki wa zamani marehemu Hemedi Maneti Ulaya Chiriku
aliyekuwa akiimba katika bendi ya umoja wa vijana Vijana Jazz enzi
hizo ambapo anasema amekuwa kwenye muziki kwa muda mrefu japokuwa kama
ilikuwa kama kujifurahisha, Komweta Hemed Maneti alianza muziki kama
kazi mwezi Agosti mwaka 2013 akiimba katika bendi ya Vijana Jazz ambayo
marehemu baba yake Mzee Hemedi Maneti Ulaya aliitumikia kwa mafanikio enzi za uhai wake.
Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku
amekuwa akijizolea umaarufu mkubwa katika bendi hiyo kwani mashabiki
wengi wamekuwa wakimkumbuka marehemu baba yake mara anapoimba jukwaani
kwani kwa kiasi kikubwa sauti zinaendana na marehemu baba yake Hemed
Maneti, Bendi ya Vijana Jazz imekuwa ikipata umaarufu siku hadi siku
katika maonyesho yake yanayofanyika kwenye klabu ya Kilwa Road Pub
Ijumaa, Jumamosi wanapiga Jet Lumo na Jumapili kwenye ukumbi wa Vijana
Hall Kinondoni.
Wanamuziki
wakongwe waliobaki kwenye bendi ya vijana Jazz ambao waliwahi kuimba na
marehemu Hemed Maneti ni Shomary Ally,Abdallah Mgonahazeru na Roshy
Mselela, Ndoto za Komweta Hemed ni kuwa mwanamuziki wa kimataifa na
kuipepeprusha vema bendera ya Tanzania ndani na nje ya mipaka ya
TANZANIA ameolewa na ana mtoto mmoja wa miaka 5 anayeitwa Fahad.
Anaongeza kuwa Changamoto za kazi ya muziki na malezi ni nyingi lakini muhimu ni kujua jinsi gani utapanga ratiba zako vizuri na kuhakikisha unafanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mtoto na hili halinishindi natimiza majukumu yangu vizuri kama mama.
Anaongeza kuwa Changamoto za kazi ya muziki na malezi ni nyingi lakini muhimu ni kujua jinsi gani utapanga ratiba zako vizuri na kuhakikisha unafanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mtoto na hili halinishindi natimiza majukumu yangu vizuri kama mama.
hata
hivyo siku za jumatatu zinakuwa zina changamoto kubwa sana hasa katika
kumwandalia mahitaji yake kwa ajili ya kwenda shule kwakuwa nakuwa
nimechoka na kazi. Mwanamuziki huyo anasema mashabiki wa bendi ya vijana
wamempokea vizuri sana kusema kweli anaongeza kuwa
"Nashukuru
Mungu sana kwa hilo na hili linajidhihirisha ninapokuwa nafanya shoo
zangu...watu hawakai chini mara nyingi wanakuwa wakicheza..." Anamaliza
kwa kusema "Umaarufu wa marehemu baba yake mzee Hemed Maneti upo na
siwezi kuuepuka...lakini kubwa watu wananipima kutokana na utendaji na
ufanisi wangu wa kazi yangu niwapo jukwaani".
KOMWETA HEMED MANETI A.K.A CHIRIKU WA VIJANA JAZZ AFUATA NYAYO ZA MAREHEMU BABA YAKE HEMEDI MANETI ULAYA
Reviewed by crispaseve
on
02:28
Rating:
Post a Comment