MSHINDI WA TUZO YA USHAIRI APATIKANA
Tuzo hizo zilianzishwa kutokana na matakwa ya mtengeneza filamu raia wa Canada, marehemu Gerlad Belkin, aliyekuwa rafiki mkubwa wa Ebrahim Hussein. Zilifanyika jana usiku katika Ukumbi wa Hotel ya New Africa iliyopo Posta, huku mgeni rasmi akiwa ni Profesa Helman Mwansoko.
Mshindi wa tuzo hizo ni Esther Mgondo kutoka Dar aliyewasilisha mashairi yaliyoitwa msamaha, changudoa na penda wewe, nafasi ya pili imechukuliwa na Rashid Rai toka Zanzibar, mashairi yake ni tamu imeingia sumu, tunda na fadhaiko, na aliyeshika nafasi ya tatu ni Sylvin Makila kutoka Mbeya na mashairi yake ni edeni, sanamu na bunge la wanyama.
Mshindi wa kwanza alijipatia kitita cha shilingi milioni mbili, mshindi wa pili aliibuka na kitita cha milioni moja na wa tatu alipata shilingi laki saba.
Gabriel Ng’osha na Gladness Mally/GPL
MSHINDI WA TUZO YA USHAIRI APATIKANA
Reviewed by crispaseve
on
07:06
Rating:
Post a Comment