BELLA AITIKISA DAR LIVE USIKU WA NANI KAMA MAMA









BENDI
ya muziki wa Dansi ya Malaika chini ya Christian Bella ‘Obama’ usiku wa
kuamkia leo iliutikisa Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo
Mbagala-Zakhem, jijini Dar baada ya kuwapagawisha mashabiki kwa shoo ya
nguvu.
Onyesho
hilo lililoanza saa tatu usiku ambapo Malaika bendi walikuwa wakiwapa
ladha mashabiki kwa kupiga kopi mbalimbali ya nyimbo za Kikongo
zinazobamba.
Ilipofika
saa nne na nusu ukumbi ulilipuka kwa shangwe baada ya kiongozi wa bendi
hiyo Christian Bella kupanda jukwaani kwa wimbo wake wa Yako Wapi
Mapenzi ambao ulisababisha mashabiki kuinuka katika viti vyao na wale
ambao walikuwa wakinyemelewa na usingizi kuamka.
Bella
alizidi kuwapagawisha mashabiki kwa kupiga nyimbo kali mfululizo ambazo
zinatamba katika redio na vyombo mbalimbali vya habari ukiwemo Nani
Kama Mama, Yako wapi Mapenzi, Msaliti, Usilie na nyingine kibao.
(PICHA/HABARI: ISSA MNALLY/ GPL)
BELLA AITIKISA DAR LIVE USIKU WA NANI KAMA MAMA
Reviewed by crispaseve
on
05:36
Rating:
Post a Comment