SHULE YA WALEMAVU BUHANGIJA JUMUISHI YAELEMEWA NA CHANGAMOTO

Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akimsikiliza kwa
makini Mkuu wa kitengo cha watoto walemavu shule ya msingi Buhangija
Jumuishi ya mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi aliyekuwa akimwelezea
changamoto mbalimbali walizonazo shuleni hapo.(Picha na Zainul Mzige).
Na MOblog, Shinyanga
SHULE
ya watoto wenye ulemavu ya Buhangija Jumuishi inakabiliwa na changamoto
kubwa zinazofanya maisha kwa watoto hao kuwa magumu. Miongoni mwa
changamoto hizo ni kukosekana kwa huduma za matibabu, walimu wa kutosha
na mabweni.
Hayo
yamebainika wakati wa ziara fupi ya Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
Tanzania, Zulmira Rodrigues. Mkuu wa Kitengo cha watoto walemavu shule
ya msingi Buhangija Jumuishi iliyopo mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi,
ndiye aliyeelezea ugumu uliopo katika shule hiyo yenye wanafunzi 209
wenye ulemavu wa aina mbalimbali.

Mkuu
wa kitengo cha watoto walemavu shule ya msingi Buhangija Jumuishi ya
mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi akimtambulisha Mkurugenzi Mkazi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues aliyefanyia ziara fupi
akiwa safarini kuelekea jijini Mwanza akiwa ameambatana na Afisa Mradi
wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias
(katikati).
Alisema
shule hiyo yenye walemavu wa aina tatu wa kusikia, ngozi na wasioona
inakabiliwa pia na lishe duni ambayo haimpi kijana nafasi ya kuendelea,
kwani wanakula mlo wa aina moja na kidogo. Shule hiyo ambayo awali
ilikuwa inawapokea wanafunzi wasioona sasa inapokea walemavu wa ngozi
kutokana na hofu iliyokuwa inalikumba taifa ya mauaji ya albino.
Aidha
mwalimu huyo alisema kwamba wameiomba serikali kuwa na muuguzi na
daktari katika makazi hayo lakini mpaka sasa hawajapatiwa kutokana na
wao wenyewe kutokuwa na uwezo wa kuwalipa. Alisema kutokana na rika
mbalimbali na tatizo la walemavu wa ngozi shule hiyo ambayo sasa
imegeuzwa kuwa makazi inastahili kuwa na daktari na mabweni yaongezwe.
SHULE YA WALEMAVU BUHANGIJA JUMUISHI YAELEMEWA NA CHANGAMOTO
Reviewed by crispaseve
on
07:02
Rating:
Post a Comment