Mkopo kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Vijana wakomboa Kikundi cha Iringa Promise Keepers

Afisa
Maendeleo ya Vijana Wilaya ya Chamwino Bw. Denis Vagela (kushoto)
akizungumza na Vijana wa kikundi cha Wajasiriamali wa Wilaya ya Chamwino
wanaojishughulisha na utengenezaji wa Sabuni za maji, Batiki na ufundi
walipotembelewa kwa ajili ya kuangalia mradi wao leo Mkoani Dodoma.
Katikati ni Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bibi Ester Riwa, na aliyekaa ni Afisa Vijana Wizara ya Habari
Vijana Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga.

Wakwanza
mbele ni Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bibi Ester Riwa akiangalia mashine ya kukamua alizeti
iliyotengenezwa na Vijana wa kikundi cha Chachu ya Maendeleo Dodoma
wakati wa kutembelea miradi ya vijana wa Mkoa wa Dodoma. Kulia ni kijana
wa kikundi hicho Bw. Ayoub Athumani.

Kijana
Samwel Nagija kutoka kikundi cha vijana cha Chachu ya Maendeleo Dodoma
kinachojishughulisha na utengenezaji wa mashine za kusaga na kukoboa,
mashine za kutengeneza matofali, mashine za kukamua alizeti, na ujenzi
wa vitanda na madawati ya chuma akiendelea na ujenzi wa mashine ya
kusaga leo Mkoani Dodoma.

Mwenyekiti
wa kikundi cha vijana cha Iringa Promise Keepers Bw. Rashid Magule
(kushoto) kinachojishughulisha na ufundi Selemala akielezea namna
kikundi chake kilivyofaidika na mkopo unaotolewa na Serikali kupitia
Mfuko wa Maendeleo ya Vijana. Wanaomsikiliza kutoka kulia ni Mwezeshaji
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa,
anayefuata ni Afisa Maendeleo ya Vijana Bi. Amina Sanga na wapili
kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw.Laurean Masele.
(Picha na Genofeva Matemu – Maelezo, Dodoma)
Mkopo kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Vijana wakomboa Kikundi cha Iringa Promise Keepers
Reviewed by crispaseve
on
10:23
Rating:

Post a Comment