Header AD

RAY J AENDELEA KUICHOKONOA NDOA YA KIMYE

Kanye Kim Ray J
Add caption
Mkali wa miondoko ya R&B na kaka wa mwanamuziki Brandy, Ray J bado ameendelea kuichokonoa ndoa ya Kim na kanye ‘KIMYE’ baada ya kutangaza dau la kununua nyumba katika mtaa wanapoishi mastaa hao.
Ray J na meneja wake, David Weintraub, wameripotiwa na mtandao wa TMZ kutangaza dau la dola milioni 2.7  katika nyumba moja iliyopo mtaa huo Ijumaa iliyopita baada ya kuithaminisha.
 Hata hivyo Ray J amesema amekuwa akiishi katika mtaa huo kwa muda mrefu kuliko Kim ambaye ni muhamihaji. 
Kipindi cha nyuma Ray J na Kim waliwahi kuwa wapenzi kabla ya mkanda wao wa ngono  kuvuja mtandaoni.  
Mwaka juzi, Ray J aliachia ngoma inayoitwa  ”I Hit it first” ambayo ilikuwa inazungumzia jinsi alivyovunja amri ya sita na Kim kabla ya kutua kwa Kanye.  Wacha Muvi iendelee
Ray J na meneja wake wakitoka kuukagua mjengo walionunua
Ray J na meneja wake wakitoka kuthaminisha mjengo waliotangaza dau la dola milioni 2.7 
Ray J na Kim enzi hizo
Ray J na Kim enzi hizo
RAY J AENDELEA KUICHOKONOA NDOA YA KIMYE RAY J AENDELEA KUICHOKONOA NDOA YA KIMYE Reviewed by crispaseve on 02:17 Rating: 5

No comments

Post AD