SIMBA MABINGWA WA KOMBE LA MAPINDUZI 2015

Mpaka dakika 90 zinamalizika sio Simba wala Mtibwa ambaye alifanikiwa kutikisa nyavu za mwenzake. Kipa
wa Simba, Ivo Mapunda ameweza kuibuka shujaa wa mchezo huo baada ya
kufuta mikwaju miwili ambayo ilipigwa na Rajab Jeba pamoja na Vicent
Barnabas wote wa Mtibwa baada ya kuchukua nafasi ya golikipa Peter
Manyika mnamo dakika ya 90.
Wakati kwa upande wa Simba wakipoteza mkwaju mmoja uliopigwa
na Shabani Kisiga na kufanya matokeo kumalizika kwa wekundu hao wa
msimbazi kuibuka bingwa kwa jumla ya mikwaju minne ya penalti dhidi ya
mitatu.
Kwa matokea hayo yanaifanya timu ya Simba kuendelea
kushikilia rekodi yake ya kuifunga Mtibwa mara mbili katika michuano
hiyo ya Mapinduzi.
Simba Sc walikabidhiwa kombe lao na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dr. Ali Mohammed Shein na zawadi
ya shilingi milioni 10 kwa kutwaa ubingwa, wakati Mtibwa ikiambulia
shilingi milioni 5 za kibongo kama zawadi ya mshindi wa pili.
SIMBA MABINGWA WA KOMBE LA MAPINDUZI 2015
Reviewed by crispaseve
on
02:11
Rating:
Post a Comment