WANAHABARI MBEYA WATEMBELEA KIWANDA CHA BIA CHA TBL NA KUSHIRIKI SHINDANO LA KUONJA BIA
Katika
shindano hilo, Mzoefu Saada Matiku ambaye ni mwandishi wa Chanel Ten
aliibuka kidedea kwa kupata alama tano kwa tano ikiwa ni mara ya pili
tangu apate nafasi kama hiyo kwenye mashindano ya mwaka juzi.
washindi
wengine ni Kenneth Ngelesi wa Tanzania Daima aliyeibuka mshindi wa pili
huku Merali Chawe wa Daily news akiibuka kidedea katika nafasi ya tatu.
Mbali
na mashindano hayo Uongozi wa Kiwanda hicho umeilalamikia Serikali kwa
kitendo cha kupandisha ushuru kwenye vinywaji katika kila mwaka wa
bajeti jambo linaloathiri uzalishaji kwa makampuni binafsi.
Hayo
yalibainishwa na Meneja wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) Kiwanda cha
Mbeya, Waziri Jemedari, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
walipofanya ziara kiwandani hapo Iyunga jijini Mbeya.
Jemedari
alisema uzalishaji wa bidhaa zao katika kiwanda cha Mbeya umepungua
kutokana na ongezeko la Kodi ambapo awali kabla ya kupandishiwa kwa kodi
hiyo Kiwanda kilikuwa kinafanya kazi masaa 24 kwa siku 7 lakini sasa
kinafanya kazi masaa 24 kwa siku tatu.
Alisema
hadi sasa uzalishaji huo umepungua kwa asilimia 40 ambapo wakati
mwingine hulazimika kuzima na kupumzisha mitambo sababu kubwa ni
kupungua kwa mauzo baada ya bei kuongezeka.
Alisema
uzalishaji ulikuwa ni Hektolita 12000 hadi 6000 kwa siku lakini sasa
hivi umeshuka hadi Hektolita 400 hivyo kusababisha hata kutishia
kupunguza watumishi.
Alisema
kitendo cha serikali kupandisha bei kwa mlaji kinaathiri pande nyingi
ambapo Mlaji mwenyewe nashindwa kumudu gharama za kununua bidhaa ili
hali mzalishaji anaweza anakazalisha kwa wingi lakini sokoni
zisinunuliwe.
“Kama
mnavyoona hizo zote ni chupa tupu ambazo zimekosa vinywaji na zilipaswa
kuwepo sokoni na hii ni kutokana na kupandisha kodi kiholela, jambo
ambalo hata Serikali haijatambua kuwa na yenyewe imekosa mapato” alisema
Meneja huyo huku akionesha chupa tupu za bia.
Aliongeza
kuwa serikali ilipaswa kumpandishia kodi mzalishaji na sio mlaji wa
mwisho jambo ambalo linaathiri uchumi wa mtu mmoja mmoja.Alisema kwa
kufanya hivyo ingekuwa rahisi kwa mzalishaji kuwa na mbinu mbadala ya
kukusanya kodi kwa ajili ya kuilipa Serikali tofauti na ilivyosasa
ambapo Serikali huongeza gharama ya kodi kwenye bidhaa inayopaswa kwenda
sokoni.
Jemedari
alisema katika kunusuru kiwanda kisifungwe uongozi wa tbl umelazimika
kupunguza bei ya vinywaji tofauti na bei elekezi inayotakiwa kutokana na
kiwango cha kodi ya serikali ambapo Bia moja ilipaswa kuuzwa 2500
lakini kiwanda kimepunguza hadi shilingi 2200.
Na Mbeya yetu
Meneja wa Kiwanda akitoa maelekezo.
|
Waandishi wa Habari wakipata maelekezo mbali mbali juu ya uzalishaji wa bia.
|
Baadhi ya Wataalamu wa Kiwanda cha Bia cha TBL wakiendelea na majukumu yao.
|
Picha ya pamoja baada ya kumaliza Ziara.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
|
WANAHABARI MBEYA WATEMBELEA KIWANDA CHA BIA CHA TBL NA KUSHIRIKI SHINDANO LA KUONJA BIA
Reviewed by crispaseve
on
01:27
Rating:
Post a Comment