Header AD

Ruhusuni wanaume wadi za leba kuchochea uzazi salama

DSC_0036
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akipitia kijarida cha maelezo kazi zinazofanywa na taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15. Kulia ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Doris Mollel wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa taasisi hiyo uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).


NAIBU Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi, Mahmoud Thabit Kombo ameitaka jamii kubadili utamaduni na kumshikirisha mwanamme wakati mke wake akienda kujifungua ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha usalama wa mtoto na mama.

Alisema wanaume wengi hasa wanawake wao wanapokuwa wajawazito na wanakaribia kujifungua wanakosa amani na wengine hukimbia nyumbani au humkimbiza mke na mtoto wao kwa ndugu na jamaa baada ya kujifungua kutokana na kukosa ushauri unaompa ujasiri kuhusu familia yake hiyo mpya.

Naibu waziri huyo alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel mwishoni mwa wiki. Alisema yeye anaamini kwamba moja ya vitu vinavyoweza kupunguza idadi ya vifo kwa watoto wa njiti ni ushiriki wa wanaume na kuwataka watu wa Doris Mollel Foundation kufanya kampeni kubwa ya kubadili tamaduni na wanaume kukalishwa chini kuelekezwa.
DSC_0069 
Muuguzi wa wodi ya watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mariana Makanda akitoa somo na elimu ya makuzi kwa watoto njiti wanaozaliwa nchini kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa taasisi hiyo.

Aidha ushiriki wa wanaume katika ujauzito umeelezwa kusaidia kuondoa mashinikizo na ukosefu wa lishe bora kwa wawanake wajawazito kutokana na vitu hivyo kuwa sehemu ya uzazi wa watoto njiti.

Alisema pamoja na kutoa elimu kwa wanaume na wanawake hasa wauguzi juu ya haja ya wanaume kuona mahangaiko ya wanawake zao, ameitaka jamii kutambua kwamba uzazi katika umri mdogo ni tatizo jingine linalopsababisha uzazi wa watoto njiti.
Alisema kuhusu mabadiliko katika hospitali na zahanati zetu ili kuwa bora kwa uzazi salama Naibu waziri huyo alitaka taasisi mbalimbali kushirikiana na serikali kuhakikisha kwamba si watoto njiti tu wanakuwa salama bali hospitali na zahanati hizo zinakuwa salama kwa uzazi wa aina zote.

Awali wakati akimkaribisha Naibu Waziri kufungua taasisi hiyo, Balozi Mwanaidi Sinare, alisema kwamba ipo haja ya zahanati na hospitali za Tanzania zikawa katika hali ya kupokea uzazi wa aina zote ili watoto njiti waweze kuendelea kuishi.
DSC_0194
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akizungumza kwenye uzinduzi wa taasisi ya Doris Mollel uliofanyika mwishoni mwa juma kwenye hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
 
Wakati huo huo mwasisi wa taasisi hiyo ambaye pia ndiye Mwenyekiti wake, Doris Mollel ambaye ni Mrembo wa Singida 2014/15, ambaye alisema kwamba yeye alizaliwa akiwa njiti na uzito wa kilio 1.2 alisema zaidi ya watoto 200,000 huzaliwa njiti kila mwaka huku elfu 9 wakifariki.
Alisema wengi wa watoto hao hufariki kwa kukosa huduma muhimu hasa mashine za kuwawezesha kunyonya, kupata joto kuendelea kuishi kabla ya kutoka hospitalini.

Alisema lengo la kuanzisha taasisi hiyo ni kutafuta fedha za kuweza kusaidia watoto njiti ili kupunguza vifo na kuviondoa. Watoto njiti milioni 15 huzaliwa duniani na kati yao milioni 1 hufa wengi wao kutoka nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania.
DSC_0112
Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akielezea makuzi yake baada ya kuzaliwa njiti wa uzito wa kilio 1.2 na kuona kuna umuhimu wa kusaidia watoto njiti wasipoteze maisha kutokana na kukosa vifaa vya kufanya watoto hao waweze kuishi na kufikia malengo kama watoto wengine ambao hawakuzaliwa na wakiwa njiti
Ruhusuni wanaume wadi za leba kuchochea uzazi salama Ruhusuni wanaume wadi za leba kuchochea uzazi salama Reviewed by crispaseve on 01:24 Rating: 5

No comments

Post AD