WAZIRI WA UJENZI DKT MAGUFULI AHITIMISHA ZIARA YAKE WILAYA YA SAME NA MWANGA MKOANI KILIMANJARO.
.jpg)
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli katikati akiweka jiwe na msingi
kuashiria kuanza kwa ujenzi wa barabara ya
Mwanga-Kikweni-Vuchama-Usangi-Lomwe yenye urefu wa kilomita 40. Kulia
kwake ni Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Mwanga Profesa Jumanne
Maghembe, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama pamoja na viongozi
wengine wa Wilaya ya Mwanga.
.jpg)
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kushoto akizungumza jambo na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe kabla ya kuweka jiwe la msingi
katika barabara ya Mwanga-Kikweni-Vuchama-Usangi-Lomwe yenye urefu wa
kilomita 40.6. Katikati ni Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Mwanga
Profesa Jumanne Maghembe.
.jpg)
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro Leonidas Gama wakicheza ngoma na kikundi cha ngoma za asili
Kikweni kabla ya uzinduzi wa barabara ya
Mwanga-Kikweni-Vuchama-Usangi-Lomwe yenye urefu wa kilomita 40.
.jpg)
.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma na kikundi cha
ngoma cha Msanja group kabla ya kuhutubia mamia ya wakazi wa Usangi
kuhusu ujenzi wa barabara ya Kikweni-Usangi-Lomwe ambayo itaanza
kujengwa hivi karibuni.
.jpg)
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kushoto akizungumza jambo na Naibu
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mama Ana Kilango Malecela katika
sehemu ya Kihurio.Dkt. Magufuli ametangaza kujengwa kilomita tatu za
lami katika eneo hilo pamoja na kuifanyia maandalizi ya kujengwa kwa
kiwango cha lami barabara ya Mkomazi-Same yenye urefu wa km 96.
.jpg)
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiwahutubia mamia ya wakazi wa Kihurio Same Mkoani Kilimanjaro.
.jpg)
Wakazi wa Usangi waliojitokeza kumsikiliza Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli
.jpg)
Waziri
wa Ujenzi akiwahutubia wakazi wa Gonja wakati akipita kukagua barabara
ya Kihurio hadi Gonja maore Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro.
.jpg)
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiagana na wananchi wa Usangi mara baada ya kuwahutubia.
.jpg)
Picha
ya Pamoja Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli katikati akiwa pamoja na
Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro
Leonidas Gama, pamoja na Viongozi wengine wa Wilaya na Chama cha
Mapinduzi mara baada ya kuhitimisha ziara yake katika Wilaya za Same na
Mwanga mkoani Kilimanjaro.Picha zote kwa Hisani ya Kitengo cha
Mawasiliano-Wizara ya Ujenzi
WAZIRI WA UJENZI DKT MAGUFULI AHITIMISHA ZIARA YAKE WILAYA YA SAME NA MWANGA MKOANI KILIMANJARO.
Reviewed by crispaseve
on
02:48
Rating:
.jpg)
Post a Comment