Header AD

KARUME DAY


 
APRILI 7 ya kila mwaka, huwa ni siku maalumu ya watanzania kuadhimisha kumbukumbu ya kuuawa kwa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Kwanza wa Baraza la Mapinduzi na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hayati Mwalimu Julius Nyerere (kushoto) na Sheikh Abeid Aman Karume wakibadilishana hati za muungano.
Huyu si mwingine, ni Sheikh Abeid Amani Karume.
Ni miaka 43 sasa, tokea kiongozi huyo alipouawa April 7, 1972 wananchi wengi wa Unguja na Pemba, bado wanasema yakini kuwa, ataendelea kukumbukwa kwa namna alivyoweza kuharakisha maendeleo ya visiwa hivyo.
Siku hii kimsingi inajulikana kama Karume Day, ambayo huwa ni ya mapumziko kwa Tanzania.
Taarifa kutoka kwa vyanzo mbalimbali vinaonyesha kuwa, Sheikh Karume alizaliwa Agosti 4, mwaka 1905 huko Mwera Zanzibar.
Kimsingi Sheikh Karume ndiye anayechukuliwa kuwa muasisi wa Zanzibar huru.
Aliviongoza visiwa hivyo, baada ya kutekelezwa mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, mwaka 1964.
Miezi mitatu baadaye, yaani Aprili 26, mwaka huo wa 1964,  pamoja na Mwalimu Julius Nyerere, Baba wa Taifa wakaziunganisha nchi zao, yaani  Zanzibar na Tanganyika  na kuwa nchi moja ya Tanzania.
Baada ya muungano, Sheikh Karume  aliendelea kuwa Rais wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu wa kwanza wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hadi alipouawa Aprili 7, mwaka 1972
KARUME DAY KARUME DAY Reviewed by crispaseve on 07:11 Rating: 5

No comments

Post AD