Rais Kikwete atoa Mhadhara katika kituo cha Kimataifa cha Woodrow Wilson
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akitoa mhadhara katika kituo cha Kimataifa cha
Woodrow Wilson (Woodrow Wilson International Centre) tarehe 3 Aprili,
2015 jijini Washington DC nchini Marekani. PICHA NA IKULU
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akifafanua jambo wakati akitoa mhadhara katika
kituo cha Kimataifa cha Woodrow Wilson (Woodrow Wilson International
Centre) tarehe 3 Aprili, 2015 jijini Washington DC nchini Marekani.
Sehemu ya wahudhuliaji katika mhadhara huo wakimpigia makofi Rais Kikwete (hayupo pichani).
Serikali
ya awamu ya nne inajivunia mafanikio iliyoyapata tangu kuingia
madarakani Mwaka 2005 na kuweka msingi imara wa nchi katika kutekeleza
Mkakati wa Maendeleo wa Mwaka 2025 (Tanzania Development Vision 2025)
ambao unalenga kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kati
ifikapo Mwaka 2025.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo tarehe 3 Aprili, 2015 jijini
Washington DC wakati akitoa mhadhara katika kituo cha Kimataifa cha
Woodrow Wilson (Woodrow Wilson Centre.
"Naamini
mrithi wangu atayaendeleza na kujifunza kutokana na mafanikio haya na
kuendeleza kutoka pale tutakapoachia" Rais amesema na kuongeza kuwa pia
anatarajia kuwa Tanzania itakuwa na sera na sheria ya kusimamia Gesi na
mapato yake kwa vile inatarajiwa kuanza kupatikana ifikapo Mwaka 2020.
Katika
mhadhara huo uliohudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo Mabalozi, wasomi
na viongozi wa taasisi hiyo, Rais Kikwete ameelezea mafanikio na
changamoto katika uongozi wake wa miaka 10 katika elimu, siasa, uchumi
na maendeleo ya jamii.
"Najivunia
kuweza kuendelea kuliweka Taifa katika hali ya Umoja pamoja na
changamoto zote, tumepambana na vitisho pale vilipojitokeza na pia
tumetoa mchango mkubwa katika harakati za kisiasa zilizopelekea vyama
viwili kutiliana saini maridhiano na kupata muafaka Mwaka 2010".
Rais
ameelezea na kuongeza kuwa makubaliano hayo yalipelekea Zanzibar
kufanya uchaguzi kwa amani na kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa baina
ya vyama vya CCM na CUF.
"Natumaini tutafanya uchaguzi huru, haki na amani ili niweze kumkabidhi
Urais mrithi wangu katika hali ya utulivu" Rais ameongeza.
Imetolewa na;
Premi Kibanga
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Washington DC - Marekani4 Aprili, 2015.
Rais Kikwete atoa Mhadhara katika kituo cha Kimataifa cha Woodrow Wilson
Reviewed by crispaseve
on
09:21
Rating:
Post a Comment