Header AD

KAMPUNI YA MSAMA PROMOTIONS YAGAWA ZAWADI ZA EIDD EL FITR KWA VITUO VYA WATOTO YATIMA JIJINI DAR

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akimkabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali kwa mtoto Sophia Said wa kituo cha Yatima cha Maunga cha Kinondoni jijini Dar es Salaam ikiwa ni masandalizi ya Sikukuu ya Idd El Fitr.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akiwakabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali watoto, Gatson Edward na Bonny Mayanga wa kituo cha Yatima cha Tuwakomboe cha Temeke jijini Dar es Salaam ikiwa ni masandalizi ya Sikukuu ya Idd El Fitir. Jumla ya vituo 10 vilinufaika na msaadahuo ambao umetokana na mapato ya Tamasha la Pasaka la mwaka huu.
Sehemu ya misaada hiyo ikishushwa


KAMPUNI ya Msama Promotions chini ya Mkurugenzi wake Alex Msama, jana iligawa misaada ya vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi mil 9.5 kwa vituo 10 vya kulea yatima vya jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi misaada hiyo kwa viongozi na wawakilishi wa vituo hivyo, Msama mwasisi wa matamasha ya Injili nchini tangu mwaka 2000, alisema ametoa vitu hivyo kuwapa faraja watoto wa vituo hivyo.

Msama ambaye hivi karibuni alitoa msaada kama huo wenye thamani ya shilingi mil 7.5, alisema msaada huo wa jana ni kuwapa faraja watoto hao kufurahia sikukuu ya Idd el Fitr inayoweza kuangukia kati ya Julai 18 au 19.

“Nimeguswa kuendelea kusaidia watoto hawa, najisikia faraja na amani ya moyo ninapofanya hivi nikikumbuka mbali mno, ikiwemo hata maisha niliyowahi kuishi na kuyapitia, hivyo si kutaka sifa wala umaarufu,” alisema.

Msama ametoa wito kwa jamii kutambua watoto wanaolelewa katika vituo hivyo si kupenda kwao, bali ni kutokana na changamoto za kimaisha zilizowapata hadi ku kila mtoto angependa kulelewa na wazazi wake.

Vituo vilivyopewa msaada wa vitu mbalimbali kama unga, mchele, sukari, sabuni na juisi, ni Honoratha, Mwana, Umra, Mujahidina, Zaidi, Hairat, Sifa, Mwandaliwa na Chakuwama.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Alhaji Mzee ambaye ni mmoja wa watoto wa kituo cha Alhaji Mzee wa kituo cha Mwandaliwa, alisema ni furaha kubwa kwao kupata msaada huo kuelekea sikukuu hiyo.

Msama alisema fedha zilizotumika kununua vitu hivyo ni kutoka katika mfuko wa Tamasha la Pasaka ambalo hufanyika kila mwaka tangu 2000 chini ya uratibu wa kampuni ya Msama Promotions.

Msama ni mtu aliyejipambanua kama mdau mkubwa katika kusaidia jamii kupitia makundi maalumu kama yatima, walemavu na wajane kwa lengo la kuwapa faraja ya kufurahia maisha kama wengine.

Mbali ya kutoa misaada mbalimbali kwa makundi hayo kabla au baada ya tamasha la Pasaka kila mwaka, Msama amewahi kusaidia waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto, mwaka 2011
KAMPUNI YA MSAMA PROMOTIONS YAGAWA ZAWADI ZA EIDD EL FITR KWA VITUO VYA WATOTO YATIMA JIJINI DAR KAMPUNI YA MSAMA PROMOTIONS YAGAWA ZAWADI ZA EIDD EL FITR KWA VITUO VYA WATOTO YATIMA JIJINI DAR Reviewed by crispaseve on 02:28 Rating: 5

No comments

Post AD