Header AD

WANASAYANSI ZAIDI YA 2000 WASHIRIKI MKUTANO WA TABIANCHI, PARIS UFARANSA

Royal CfCC15.jpgwPichani: Baadhi ya Wanasayansi wakifuatilia mawasilisho ya wanasayansi wenzao yaliyokuwa yakiwasilishwa katika mkutani huo ulioanza Julai 7 na kumalizika Julai 10, mwaka huu katika ukumbi mkubwa wa makao makuu ya UNESCO, Paris, Ufaransa.

Na Andrew Chale, Modewjiblog
[Paris, Ufaransa] Wanasayansi zaidi ya 2500, kutoka pembe zote duniani wamekutana katika mkutano mkubwa wa wanayasansi juu ya siku za usoni na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ‘Our Common Future Under Climate Change’. 

Mkutano huo ulioandaliwa katika makao makuu ya UNESCO mjini Paris, Ufaransa, ulikuwa wa siku nne (Julai 7-10) na ndio ulikuwa mkutano mkubwa zaidi wa wanasayansi duniani kuanda makataba ambao unatarajiwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi utakaofanywa hapo Desemba, mjini Paris.

Ushiriki wa wanasayansi hao katika mkutano wao huo umefanya jiji la Paris kuwa na pilikapilika za hapa na pale hasa viunga vya makao makuu ya UNESCO na yalipokuwa yanafanyika matukio ya mkutano huo.

Miongoni mwa mada zilizowakilishwa katika mkutano huo ni pamoja na namna ya dunia itakavyokabiliana na kiwango cha hali ya joto na nyuzi mbili (to reduce temperature level by 2 degrees), mafuliko yanayokumba nchi mbalimbali duniani (Floods). Mada zingine ni kama vile misitu, athari za watu kuongezeka mijini, ongezeko la joto, kupungua kwa vina vya bahari, masuala ya hewa ukaa, gesi sumu na mengine mengi yanayopelekea athari za tabianchi.

Mkutano huu ulilenga jinsi ya kukabiliana na tabianchi pamoja na kubadilishana ujuzi zaidi hii ikiwa ni kuelekea mkutano mkuu wa 21 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiriko ya Nchi (COP21) utakaofanyika hapa hapa Paris , Desemba mwaka huu.

Hata hivyo matarajio ya wanasayansi wengi wakiwemo kutoka nchi tofauti wameeleza kuwa, hadi kufikia mkutano wa COP 21, hiyo Desemba mataifa yataafikiana maamuzi ya kila mmoja wapo pindi watakapo wasilisha.
18898203484_c8cbf79953_kBaadhi ya wanasayansi wakiendelea na mkutano katika moja ya kumbi za mikutano katika viunga vya Makao makuu ya UNESCO, Paris Ufaransa.
WANASAYANSI ZAIDI YA 2000 WASHIRIKI MKUTANO WA TABIANCHI, PARIS UFARANSA WANASAYANSI ZAIDI YA 2000 WASHIRIKI MKUTANO WA TABIANCHI, PARIS UFARANSA Reviewed by crispaseve on 02:34 Rating: 5

No comments

Post AD