YOLANDA SHAYO BALOZI WA MKOA WA KILIMANJARO ATEMBELEA VITUO VYA WATOTOTO YATIMA
Mrembo
aliebuka kidedea kwenye shindano la kumsaka barozi wa mkoa wa
Kilimanjaro 2015,Yolanda Shayo ametembelea vituo vya watoto yatima
katika eneo la mamba Malangu moshi vijijini.
Shughuli
hiyo ilifanyika mapema jana ambapo mrembo huyo alitembelea vituo vinee
ambavyo ni Msoroe,Mrieni,Kikoro na kotela kwa kugawa vifaa vya shule kwa
watoto na kula nao chakula cha pamoja kilichoandaa kwaajili ya watoto
hao.
Baadhi
ya vitu vilivyotolewa na mrembo huyo ni kalamu,madaftari,rula na sabuni
za kufulia na kuogea,Yolanda alipata fulsa ya kuongea na viongozi wa
vituo hivyo ambapo alibaini changamoto balimbali zinazokabili vituo
hivyo.
Yolanda
ambae ni Miss Kilimanjaro Ambassador wa mara ya kwanza ameonesha
jitihada zake za kuanza kazi ya urembo kwa kuitumikia jamii yake ambapo
alikuwa ana wito huo tangu akiwa mtoto.
Kwa
nafasi aliyoipata mrembo huyo ameaidi kuwa kinara kuutangaza utamaduni
wa mkoa wa kilimanjaro na kuvitangaza kitaifa na kimataifa vivutio vya
utalii vilivyomo ndani ya mkoa huo.
"mbali
ya kuwa mrembo na balozi wa mkoa wa kilimnjaro nitahakikisha natumia
fulsa hii kupeleka ujumbe mbalimbali kwa jamii yangu ikiwemo kuwahimiza
vijana wenzangu kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura katika uchaguzi
mkuu utakaofanyika octoba" aliongea Yolanda.
YOLANDA SHAYO BALOZI WA MKOA WA KILIMANJARO ATEMBELEA VITUO VYA WATOTOTO YATIMA
Reviewed by crispaseve
on
08:59
Rating:
Post a Comment