SERIKALI KUFANYIA KAZI MAPENDEKEZO YA WASAFIRISHAJI
Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii
Serikali
imejipanga kufanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na jukwaa la
usafirishaji nchini ,ili kuboresha hali ya usafiri hapa nchini kutoka
bandarini kutoka nchini jirani.
Hayo
yamesemwa na Katibu mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na uchukuzi,Profesa
Faustine Kamuzora alipokuwa akifungua jukwaa hilo lililoasisiwa na
tasisi ya Trade Mark East Afrika.
"Hivyo
serikali imejipanga na kuakikisha kuwa bandari ya Dar es Salaam inakuwa
sehemu rafiki kwa wafanyabiashara kutoka nchi zinazotunguka kwa
kupunguza urasimu unaochangia kuchelewa kwa kutoa mzigo
bandarini"amesema Prof Kamuzora
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa hilo la usafirishaji ,Angelina Ngalula
, amesema kuwa serikali inatakiwa kuanza kuandaa mazingira ya
upatikanaji wa mzigo wa tani milioni 10 katika reli ya Standard Geji
inayo taraji kujengwa hapa nchini .
Amesema
kuwa wazo la serikali la kujenga reli ya kisasa ni zuri hivyo tunaiomba
serikali inahakikisha inaandaa mazingira ya upatikanaji wa mizigo hili
tusije tukaiona reli hiyo kama pambo tu.
Mkurugenzi
mkazi wa Trademark East Afrika,John Ulanga akizungumza na wadau wa
usafirishaji wakati uzinduzi wa jukwaa lamusafirishaji.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TPSF ,Godfrey Simbeye akito maelezo jinsi tasisi yake
inavyofanya kazi bega kwa bega na wawekezaji ususani katika swala la
usafirishaji.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Usafirishaji ,Angelina Ngalula akizungumza na wadau wa usafirishaji wakati uzinduzi wa jukwaaa hilo.
Katibu
mkuu wa wizara ya Uchukuzi,Prof Faustine Kamuzora akitoa hotuba ya
ufunguzi wa jukwaa la usafirishaji jijini Dar es Salaam
Wadau wa usafirishaji wakisikiliza kwa makini wakati wa uzinduzi wa jukwaa hilo.
Picha ya pamoja ya wadau wa usafirishaji na mgeni rasmi.
SERIKALI KUFANYIA KAZI MAPENDEKEZO YA WASAFIRISHAJI
Reviewed by crispaseve
on
04:14
Rating:
Post a Comment