Header AD

WAFANYABIASHARA WA VIUMBE PORI HAI WAOMBA HURUMA YA RAIS MAGUFULI.



Na Ally Daud-MAELEZO

WAFANYABIASHARA wa viumbe pori hai wamemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kufungulia biashara ya viumbe hao kutokana na kusitishwa Machi mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii Jumanne Magembe.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Viumbe pori hai Bw. Salim Mussa amesema kuwa wanamuomba Mh. Rais Magufuli aingilie kati swala hilo na kupata ufumbuzi wa kudumu wa kuendelea na biashara hiyo ya viumbe kwa maendeleo yao na uchumi wa taifa.

“Tunakuomba Mh. Rais Magufuli uingilie kati swala hili na kutupatia ufumbuzi wa kudumu ili kuendlea na biashara ya viumbe pori hai bila ya usumbufu wa mara kwa mara kwani biashara hii ipo kwa mujibu wa sheria , taratibu na kanuni za nchi” alisema Bw. Salim.

Aidha Bw. Salim amesema kuwa maamuzi hayo yanaweza kusababisha hasara kubwa kwa jumuiya ya wafanyabiashara wa viumbe hivyo na uchumi wa nchi kwa ujumla kwani muongozo haujatolewa tangu kusitishwa kwa biashara hiyo mwezi machi mwaka huu.

Kwa upande wake Msemaji wa wafanyabiashara wa viumbe pori hai Bw. Enock Balilemwa amesema kuwa kusitishwa kwa biashara hiyo imepunguza kiwango cha ajira kwa kiasi cha watanzania milioni moja ambao asilimia 95 wanaishi vijijini.

“kusitishwa kwa biashara hii ya viumbe pori hai imefanya watanzania takribani milioni moja hasa wakazi wa vijini asilimia 95 kukosa ajira jambo ambalo linapelekea wananchi hao kukosa uwezo wa kujikimu kwa maisha ya kila siku” alisema Bw. Balilemwa.

Biashara hiyo ya viumbe pori hai inayojumuisha Vyura, wadudu, ndege,mijusi na tumbili, zoo na mashamba ya wanyapori ilianza kabla ya uhuru sambamba na leseni zingine za uwindaji wa kitalii ambayo mpaka sasa inatambulika kwa sheria namba 5 ya mwaka 2009.
WAFANYABIASHARA WA VIUMBE PORI HAI WAOMBA HURUMA YA RAIS MAGUFULI. WAFANYABIASHARA WA VIUMBE PORI HAI WAOMBA HURUMA YA RAIS MAGUFULI. Reviewed by crispaseve on 01:54 Rating: 5

No comments

Post AD