MAONI YA WATEJA NI MUHIMU KWA UKUAJI WA BIASHARA YAKO
Na Jumia Travel Tanzania
KUJA
kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia hususani mtandao wa intaneti
kumebadilisha kwa kiasi kikubwa mienendo ya matangazo ya utoaji wa
huduma mbalimbali duniani na hii ni kutokana na uwezo wake wa kuwaruhusu
wateja kutoa ushuhuda, kukosoa au kutoa maoni juu ya walichohudumiwa na
kujionea.
Tofauti
na kipindi cha nyuma kidogo ambapo wataalamu wa masoko walikuwa
wanatumia zaidi njia za luninga na redio kuwafikia wateja wao, siku hizi
mfumo wa intaneti unapewa kipaumbele zaidi kutokana na namna
unavyofikia watu wengi zaidi ndani ya muda mfupi, kwa haraka na gharama
kidogo.
Matangazo
ya luninga na redio yanaweza kuwa hayana ushawishi mkubwa ukilinganisha
na mtandao wa intaneti kwani hivi sasa makampuni yanaweza kuwasilisha
bidhaa na huduma zao na kupokea majibu kujua kwamba zinakubalika au la.
Hali hiyo ni dhahiri kutokana na makampuni mengi kuwekeza kwa kiasi
kikubwa katika teknolojia na rasilimali watu katika kusimamia tovuti na
kurasa zao rasmi za mitandao ya kijamii kama vile facebook, twitter,
instagram na mingineyo.
Kupitia
tovuti na kurasa hizo za mitandao ya kijamii biashara na huduma nyingi
zinafanya vizuri kutokana na ushawishi wao kwenye mitandao kutokana na
namna ambavyo zinazungumziwa vizuri na watu wengi. Lakini pia husaidia
kampuni hizo husika kuwasiliana moja kwa moja na wateja wao kwa sababu
wateja huwasilisha maoni yao moja kwa moja mtandaoni tofauti na luninga
au redio ambazo hutoa fursa ya kuona au kusikiliza tu matangazo.
Vivyo
hivyo hali hii inaweza kusaidia sana ukuaji wa sekta ya utalii na
ukarimu kama vile huduma za hoteli na malazi ambazo hujitangaza zaidi
kupitia namna wateja wanavyozizungumzia.
Jumia
Travel (www.travel.jumia.com) kampuni unaongoza kwa huduma za hoteli
mtandaoni barani Afrika umezitunuku vyeti hoteli kadhaa ambazo
zilizopendekezwa na kutembelewa ndani ya wateja wengi kipindi cha mwaka
mzima wa 2016.
Akizungumzia
juu ya umuhimu wa vyeti hivyo Meneja Mkazi wa Jumia Travel Tanzania,
Bi. Fatema Dharsee amesema kuwa, “Vyeti hivi vina umuhimu mkubwa kwani
ni viashiria vikubwa vya namna hoteli yako inatathminiwa vipi na wateja
pindi wanapoitembelea. Siku zote wateja huambizana huduma wanazozipata
sehemu za biashara wanazotembelea na kutokana na ushuhuda huo ndio na
wengine hushawishika kutembelea pia. Kupitia mtandao wetu wateja
wanayofursa ya kutoa maoni juu ya hoteli walizozitembelea, huduma
walizopatiwa, mapungufu waliyoyaona na maboresho ambayo wangependa
yafanyiwe kazi.”
“Imefikia
mahala sasa ni lazima wataalamu wa masoko watambue mchango na ushawishi
walionao wateja kwenye kukua kwa biashara zao kwani nguvu yao ni kubwa
zaidi ya matangazo wanayoyalipia kupitia luninga na redio au njia
nyinginezo. Maneno au ushuhuda unaotolewa na wateja unatosha kwa kiasi
kikubwa mtu kutumia bidhaa au huduma yako kwani ni halisi kutokana na
mtu kuitumia au kupatiwa huduma hiyo husika. Hivyo ningependa kutumia
fursa hii kuwataka mameneja wa hoteli waliokabidhiwa vyeti hivi
kuichukulia hali hii kama ni changamoto kwao kwa kufuatilia maoni ya
wateja yanayoachwa kwa njia ya mtandao na kuyafanyia kazi.” Alihitimisha
Bi. Dharsee.
Hoteli
ambazo zimepatiwa vyeti hivyo ni pamoja na Jafferji House & Spa
Hotel na Garden Lodge za visiwani Zanzibar, Golden Tulip Hotel, Peacock
Hotel na Butterfly Hotel zote za jijini Dar es Salaam.
MAONI YA WATEJA NI MUHIMU KWA UKUAJI WA BIASHARA YAKO
Reviewed by crispaseve
on
10:08
Rating:
Reviewed by crispaseve
on
10:08
Rating:


Post a Comment