MKUU WA WILAYA YA ILALA, SOPHIA MJEMA AKABIDHI ZAWADI ZA KAPU LA SIKUKUU JIJINI DAR ES SALAAM
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (katikati), akimkabidhi zawadi msanii Irene Paul.
Maelekezo ya upokeaji wa zawadi hizo yakitolewa.
DC Mjema akizungumza na wanahabari baada ya kukabidhi zawadi hizo.
Washindi wa shindano hilo wakiwa katika picha ya pamoja.
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Alpha Joseph (kulia) akimkabidhi zawadi Kelvin Mhenzi
Washindi wakiondoka na zawadi zao.
Na Dotto Mwaibale
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema
ametoa zawadi mbalimbali kwa washindi 24 wa shindano la Kapu la Sikuu
lililoendeshwa na Kampuni ya Multichoice Tanzania na Kituo cha Redio cha
EFM.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi
zawadi hizo Dar es Salaam leo DC Mjema aliwataka wananchi kuendelea
kufuatilia kwa karibu vipindi mbalimbali vinavyotangazwa na kituo hicho
ili waweze kujipatia zawadi kutokana na kujibu maswali yatokanyo na
vipindi hivyo na kuweza kupata zawadi kama walizopata wenzao katika
kipindi hiki cha Sikukuu.
"Napenda kuwapongezwa EFM kwa shindano
hili kwani linatoa msukumo kwa wananchi wa kusikiliza vipindi mbalimbali
vyenye manufaa" alisema Mjema.
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania,
Alpha Joseph akizungumza katika hafla hiyo alisema kampuni hiyo kupitia
kisambuzi chake cha DSTV imemwaga zawadi ya visambuzi vya kisasa
vipatavyo 24 pamoja na vifurushi vya mwezi mzima kwa washindi wa
shindano hilo la Kapu la Sikuu.
"Washindi hao wataweza kusherehekea
Sikukuu ya krismas na mwaka mpya kwa kuangalia chaneli zaidi ya 70 za
DStv ikiwemo mpira wa ligi ya Hispania (Laliga) na ligi ya Uingereza"
alisema Joseph
Alpha alisema Multichoice Tanzania
haijawatunuku washindi hao 24 wa kapu la Sikuu pekee bali watanzania
wote kwa ujumla kwani hivi karibuni walishusha bei za vifurushi vyao kwa
wastani wa asilimia 16, huku kifurushi maarufu cha DStv Bomba chenye
chaneli zaidi ya 70 kikipunguzwa bei hadi sh.19,975 tu.
Zawadi hizo kwa washindi hao zilitolewa
na wasanii waigiza maarufu nchini kama Muhogo Mchungu, Riyama Ali, Haji
Salum Mboto na Hashim Kambi wanaoonekana katika Tamthilia ya Huba.
MKUU WA WILAYA YA ILALA, SOPHIA MJEMA AKABIDHI ZAWADI ZA KAPU LA SIKUKUU JIJINI DAR ES SALAAM
Reviewed by crispaseve
on
07:01
Rating:

Post a Comment