BILIONI 251 ZATENGWA KUIMARISHA HUDUMA ZA DAWA KATIKA VITUO VYA AFYA.
SERIKALI
kupitia Wizarya afya , maendele ya jamii , Jinsia Wazee na Watoto
imetenga bilioni 251 ili kuimarisha upatikanaji wa dawa katika vituo vya
afya na zahanati zote nchini .
Hayo
yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara Ya Afya, Maendeleo Ya Jamii, Jinsia,
Wazee Na Watoto Dokta Mpoki wakati wa mahojiano katika kipindi cha
Tunatekeleza kinachoendeshwa na kituo cha matangazo TBC1 jijini Dar es
salaam.
“Kutokana
na taarifa zinazozagaa juu ya upungufu wa dawa katika zahanati hapa
nchini ,taarifa hizo si za kweli napenda kuwatoa hofu wananchi na bajeti
yetu ya mwaka huu ni shilingi Bil. 251 kwa ajili ya dawa tu” alisema
Dkt. Ulisubisya
Aidha
Dkt. Ulisubisya alisisitiza kuwa kuna dawa zitapewa kipaumbele kutokana
na mahitaji yake kuwa makubwa nchini ukilinganisha na mahitaji ya dawa
nyingine hivyo dawa zote zitaendelea kuwepo ili kuwasaidia wananchi wote
wenye uhitaji.
Dkt.
Ulisubisya aliweka wazi juu ya mipango ya serikali katika kuimarisha
huduma za afya katika maeneo mbali mbali nchini ili kujenga taifa lenye
watu imara kiafya.Kwa
mujibu wa Dkt. Ulisubisya amesema kuwa vituo vya serikali na vya watu
binafsi ni vyema viendelea kufuata sera, taratibu na sheria ikiwemo bei
elekezi katika kuwahudumia wananchi huduma bora kwa gharama ndogo.
Dkt.
Ulisubisya amesisitiza kuwa Kufikia mwezi wa tano mwaka huu asilimia 90
ya dawa zote zitakua zimepatikana na kusambazwa kwenye vituo vya afya na
zahanati zote nchini ili kuimarisha sekta ya afya na mpaka sasa chanjo
zote zipo za kutosha.
“Tunataka
kila kituo cha afya kinachojengwa sasa hivi kitoe huduma za upasuaji
ili kupunguza mlundikano wa wagonjwa wanahoitaji huduma hiyo na kuokoa
maisha ya mtanzania kwa haraka zaidi alisema Dkt. Ulisubisya.
Aidha
Dkt Ulisubisya alisema kuwa Serikali ina mkakati wa kuimarisha huduma
zote za vipimo ili zipatikane katika hospitali za wilaya na kikanda
mpaka kufikia 2020 ili kuwezesha taifa kupiga hatua katika sekta ya
afya.
BILIONI 251 ZATENGWA KUIMARISHA HUDUMA ZA DAWA KATIKA VITUO VYA AFYA.
Reviewed by crispaseve
on
07:20
Rating:
Post a Comment