ANZIA : KIFO CHA SETH KATENDE (BIKIRA WA KISUKUMA)
Kwa
majonzi makubwa, uongozi na wafanyakazi wote wa Efm radio na tv-E ,
unasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi mwenzetu Seth Katende –
maarufu kama bikira wa kisukuma kilichotokea Julai 9 katika hospitali ya
taifa Muhimbili.
Ni
vigumu sana kuamini na kukubali msiba huu mzito kwetu lakini kwakuwa
sisi ni binadamu na kila nafsi lazima ionje umauti, tunamuomba mwenyezi
mungu aipumzishe roho ya marehemu mpendwa wetu seth katende mahali pema,
Amina.
Uongozi
na wafanyakazi wa Efm radio na tv-E unatoa pole kwa familia ya marehemu
na wasikilizaji wetu wote walioguswa na msiba huu.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe, Amina.
ANZIA : KIFO CHA SETH KATENDE (BIKIRA WA KISUKUMA)
Reviewed by crispaseve
on
05:23
Rating:
Post a Comment