MANTRACK TANZANIA YAONESHA MAPINDUZI MAPYA YA TEKNOLOJIA KATIKA SEKTA YA UJENZI NCHINI.
Katika
kuunga juhudi za Serikali ya awamu ya tano ya kuleta maendeleo kwa
wananchi kampuni ya magari ya Mantrack Tanzania jana imeendesha warsha
fupi yenye lengo la kutambulisha vifaa na teknolojia mpya itakayoongeza
ufanisi wa kazi hasa katika sekta ya ujenzi.
Akizungumza
na waandishi wa habari, mwakilishi wa kampuni ya Mantrack Tanzania
alisema kuwa wameleta vifaa vipya vitakavyoendana na kasi ya maendeleo
ya Serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha Tanzania mpya inajengwa na
uchumi bora na yenye miundombinu bora.
“Vifaa
hivi ni imara na vinatumia teknolojia mpya na ya kisasa inayosaidia
utendakaji wa shughuli za ujenzi kuwa rahisi. Tumeamua kuja na kasi ya
serikali mpya ya kutenda vitu kwa urahisi na kwa ufanisi wa hali ya
juu”.
Tuna
wakaribisha wadau wa ujenzi wafike kujionea wenye tunachosema. Alisema.
Warsha hiyo imefanyika katika karakana ya Mantrack Tanzania iliyopo
karibu na jengo la Quality Plaza barabara ya Nyerere na ilihudhuriwa na
wadau mbalimbali kutoka makampuni mbalimbali ya ujenzi hapa nchini
waliofika kushuhudia vifaa hivyo vinavyofanya kazi.
MANTRACK TANZANIA YAONESHA MAPINDUZI MAPYA YA TEKNOLOJIA KATIKA SEKTA YA UJENZI NCHINI.
Reviewed by crispaseve
on
08:33
Rating:
Post a Comment