Mkuu
wa wilaya ya Morogoro mjini, Regina Chonjo (katikati) akikata utepe
kuzindua kisima kilichotolewa msaada na kampuni ya Tigo chenye thamani
ya shilingi milioni 17/- kwa hospitali ya Mji mpya jana mjini Morogoro.
Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Meneja wa huduma za jamii Tigo, Halima Okash, Ofisa Mkuu wa Ufundi na Taarifa wa Tigo (CTIO) Jérôme Albou, na Diwani wa mji mpya Wence Kalogelezi
|
Mkazi
wa Mji mpya akiwa kabeba ndoo ya maji mara baada ya uzinduzi wa kisima
kilichotolewa msaada na kampuni ya Tigo chenye thamani ya shilingi
milioni 17/- kwa hospitali ya Mji mpya jana mjini Morogoro.
Mkuu
wa wilaya ya Morogoro mjini, Regina Chonjo (katikati) akihutubia wakazi
wa Mji mpya mara baada ya kuzindua kisima kilichotolewa msaada na
kampuni ya Tigo chenye thamani ya shilingi milioni 17/- kwa hospitali ya
Mji mpya jana mjini Morogoro.
Mkuu
wa wilaya ya Morogoro mjini, Regina Chonjo akiwa katika picha ya pamoja
na Wakazi wa Mji Mpya Mkoani Morogoro mara baada ya uzinduzi w kisima
hicho. kisima
kilichotolewa msaada na kampuni ya Tigo chenye thamani ya shilingi
milioni 17/- kwa hospitali ya Mji mpya jana mjini Morogoro. |
·
Uchangiaji huu ni ishara ya shukurani
kwa wakaazi hao kwa kuzima moto katika kituo cha data cha Tigo.
Tarehe 27 Julai 2017 – Tigo Tanzania imechangia kisima chenye thamani ya TZS milioni 17 kwa
hosipitali ya Mji Mpya na maeneo yanayoizunguka katika mkoa wa Morogoro kama
mkono wa shukurani kwa wakaazi kwa kuhatarisha maisha yao wakati wakipambana na
moto ambao ulilipuka katika kituo cha data cha kampuni katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa Tigo, uchimbaji wa kisima hicho pia ulikuwa sambamba na nia
ya kampuni hiyo kusaidia ustawi wa jamii ambako Tigo inaendesha shughuli zake.
Akizungumza
katika sherehe za makabidhiano zilizofanyika katika hospitali ya mji mpya katika
manispaa ya mji wa Morogoro Afisa Ufundi na Taarifa wa Tigo (CTIO) Jerome Albou
alielezea matarajio yake kwamba kisima hicho kitawafikisha mbali sana katika kuondoa
suala la upungufu wa maji katika hospitali na pia kutoa maji safi na salama ya
uhakika kwa jamii inayokizunguka.
“Tunawashukuru
sana watu wa Mji Mpya kwa kuonesha kujali na kujitoa wakati wa kupambana na
moto ambao karibu uteketeze kabisa kituo cha Data mapema mwaka huu. Kweli Tigo
ina deni kwa wanajamii, serikali ya mtaa na viongozi wa ulinzi na usalama wa manispaa
kwa kuitika kwa wakati kuhakikisha kuwa
hakuna uharibifu mkubwa unasababishwa wakati wa moto,” alisema Albou.
“Kwa hiyo
msaada huu, unakuja kutimiza ahadi walioiweka Tigo kwa wakazi wa Mji mwema wa
kuwapatia maji safi na salama kama namna ya kutambua juhudi zao katika kulinda
mali za kituo hicho cha data.”
Albou alibainisha
kwamba uchangiaji huo unakamilisha idadi ya vijiji 20 ambavyo vimenufaika kutokana
na jitihada za Tigo za kutoa maji safi na salama nchi nzima, ikiwa inawasaidia zaidi
ya watu 187,000.
Mwaka huu, Tigo ina mpango wa kuchimba visima zaidi
katika maeneo yanayohitaji ambayo zaidi ya watu 350,000 wanatarajiwa kunufaika katika
jitihada zetu za kusaidia juhudi za serikali za kuondoa upungufu wa maji safi
na salama nchini.
Makabidhiano yalishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro Dr Kebwe Stephen Kebwa ambaye aliishukuru Tigo kwa kufikiria kutoa
msaada huo. Alisema kwamba kisima hicho kitasaidia utoaji wa huduma bora za
kiafya katika hospitali ya Mji Mwema na kusaidia katika maendeleo ya kiuchumi
na kijamii. Aliwaomba wasamaria wema wengine kujitokeza na kuunga mkono juhudi
za kuondoa upungufu wa maji katika mkoa huo.
Tunapenda kuishukuru Tigo kwa
kutusaidia katika juhudi zetu za kutoa huduma za kiafya za uhakika katika eneo
hili kwa kutatua tatizo lililokuwepo la upungufu wa maji. Tunaamini kwamba upatikanaji
wa maji safi na salama karibu na wakaazi pia itaongeza uzalishaji wa kiuchumi
hasa kwa wasichana na wanawake ambao hawatakuwa wanapoteza muda mwingi wa
kutafuta maji safi na salama sehemu zingine. Hii itawapatia wasichana fursa ya
kuhudhuria masomo kwa uhuru na kuipa jamii fursa ya kuhudhuria kwa ufanisi katika
shughuli zao za maendeleo ya Taifa, Alisema Dr Kebwe.
|
Post a Comment