Maendeleo ya miundombinu: Nguzo ya uwezeshaji katika kufikia uchumi imara
Wananchi wa Kahama wakishuhudia uzinduzi wa safari za ndege za shirika la Precision Air katika uwanja wa ndege wa Buzwagi. |
Mazingira
mazuri ya kukuza uchumi yanahitaji miundombinu bora inayowezesha
uchukuzi huku ikiboresha uzalishaji na ufanisi. Hivi karibuni, wakazi wa
Kahama na Shinyanga watafurahia safari za ndege kati ya Kahama na Dar
es Salam. Haya ni matokeo ya ushirikiano wa Acacia Mining ulioanza toka
mwaka 2008, ilipoanza uzalishaji katika mgodi wake wa Buzwagi; huku
wakiendelea kuwekeza katika kiwanja cha ndege cha Kahama, wakihakikisha
kiwanja kinatunzwa na kufanya kazi.
Ushirikiano wa karibu kati ya Mkuu wa Wilaya Mh. Fadhil Nkurlu na Mgodi umewezesha kuanzishwa kwa safari za ndege za moja kwa moja. Safari za shirika la ndege la Precision zitapunguza adha ya usafiri ya wakazi wa Kahama na Shinyanga waliotakiwa kusafiri hadi Mwanza ili kupata usafiri wa ndege kuelekea Dar es Salaam.
‘Hii itasaidia sana kuongeza ufanisi katika muda na fedha zinazotumika katika usafiri,’ alisema mfanyabiashara Bw. Charles Thomas akiongeza kuwa safari ya barabara hadi Mwanza ingeweza kuchukuwa hadi masaa 6. Kufuatia mafanikio ya safari ya majaribio mwezi uliyopita, Meneja Mahusiano wa Kampuni wa shirika la ndege la Precision, Bw. Hillary Mremi alisifia hali ya kiwanja akisema, ‘njia ya ndege kwenye kiwanja cha ndege cha Buzwagi ipo katika hali nzuri na matunzo yake ni mazuri; hii ni nzuri kwa usalama wa abiria na ndege zetu.
Tunashukuru Acacia kwa kuwekeza katika kuboresha, kiwanja kidogo cha Buzwagi; hatua iliyoturuhusu kuanza safari kuelekea Kahama, zitakazo anza 5 September, 2017, tukiwa na safari tatu kwa wiki, na safari zikiongezeka zikitegemea mahitaji ya wasafiri. Hatua ya kutatua shida ya miundombinu ni moja itakayoleta matokeo chanya kwa biashara mkoani Shinyanga kwa kupunguza gharama za kuendesha biashara; huku ikiongeza faida.

Japokuwa
Acacia imefanya uwekezaji wenye tija katika kuendeleza na kurekebisha
kiwanja hiki kidogo cha ndege, ni muhimu kukumbuka kwamba kiwanja hiki
ni mali ya Serekali chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA). Uwekezaji katika kiwanja hiki kidogo inaonyesha nia ya
Acacia kuendelea kusaidia jamii na taasisi zinazozunguka migodi yake.
Maendeleo ya miundombinu: Nguzo ya uwezeshaji katika kufikia uchumi imara
Reviewed by crispaseve
on
11:08
Rating:
Post a Comment