Manispaa ya Sumbawanga watakiwa kujenga vituo vya afya zaidi
Waziri
wa Afya Ummy Mealimu akiongea na mmoja wa wagonjwa waliofika kupata
matibabu kwenye kituo cha afya cha Mazwi kilichopo Manispaa ya
Sumbawanga
Waziri Ummy mwalimu akimuuliza mmoja wa mama aliyefika kupata matibabu ya nje kwenye kituo cha afya cha Mazwi kama amefika muda mrefu na hajapata matibabu,waziri huyo yupo mkoani Rukwa kwa ajili ya ziara ya kikazi ya kukagua huduma za afya zinazotolewa kwenye vituo vya huduma nchini
Waziri Ummy Mwalimu akiongea na mama mjamzito aliyelazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Rukwa.Waziri Ummy alisisitiza watoa huduma kuhakikisha awatoa huduma wa afya wanajitahidi kuepusha vifo vianavyoweka kuepukika kutokana na uzazi
Waziri wa Afya akiongea na akina mama wajawazito waliolazwa kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Rukwa
Waziri akimjulia hali mama mjamzito aliyelezwa kwenye kituo cha afya katika manispaa ya Sumbawanga
Moja ya kipaumbele cha wizara ya afya katika kuokoa vifo vya akina mama wajawazito wakati wa kujifungua ni Damu Salama,Waziri wa Afya akiangalia akikagua bank ya damu salama iliyopo kwenye hospitali ya rufaa ya Mkoa
Baadhi ya watumishi wa sekta ya afya wa manispaa na mkoa wa Rukwa wakimsikiliza waziri wa afya(hayupo pichani) wakati wa kuongea na watumishi hao ambao walitoa changamoto zao zinazowakabili katika utendaji kazi zao za kila siku
Mmoja wa watumishi wa kada ya afya akiulizwa swali wakati wa mkutano wa majumuisho ya ziara ya waziri huyo.Waziri wa afya yupo mkoani Rukwa kikazi ambapo aliweza kutembelea vituo vya afya na hospitali zilizopo wilaya za Nkasi,Kalambo ,Manispaa ya Sumbawanga na hospitali ya Mkoa ya Rukwa(picha zote na Wizara ya afya)
………………………………………………………………
WAMJW- Rukwa
Manispaa ya Sumbawanga imeelekezwa kuongeza kujenga vituo vya afya kulingana na jiografia ilivyo ili hospitali ya Rufaa ya mkoa ibaki kutoa huduma za kibingwa mkoani hapa.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akiongea na watumishi wa sekta ya afya wa Mkoa na Wilaya kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wakati wa majumuisho ya ziara ya siku mbili ya kikazi
Alisema Serikali inaboresha hospitali za Rufaa za Mkoa kwa ajili ya huduma za kibingwa hivyo hospitali hizo ziweze hutoa huduma za kimatibabu ya kibingwa hasa kwa watu wenye huitaji huo,”lakini wananchi wanapaswa kufuata utaratibu wa sera unavyosema kwenda kupata matibabu katika hospitali za Rufaa ni lazima mgonjwa aandikiwe rufaa na sio kila mtu anaenda moja kwa moja kwenye hospitali hizo”
Waziri Ummy alisema kulingana na kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini ni vyema na mkoa kwa ujumla ni vyema kujenga vituo hivyo vitakavyoweza kutoa huduma kwa wananchi waliopo maeneo husika kuliko kujenga hospitali ya Wilaya ambayo wananchi waliopo maeneo ya mbali wapate huduma za afya huko huko karibu na huduma hizo ziwe bora.
“Fanyeni maamuzi yenye manufaa kwa wananchi wa wilaya yenu ili muwasogezee huduma watu wenu,alisema kwa Wilaya ya Nkasi wao wanatakiwa kujenga hospitali ya wilaya ya serikali ambapo Wizara yake itasaidia kutoa milioni 350 kati ya 650 ambayo itajenga wodi ya wazazi,maabara pamoja na nyumba moja ya mtumishi
Aidha,kwa Wilaya ya Kalambo alisema wanatakiwa kuboresha kituo cha afya Bimbwi kwa kujenga chumba cha dharura cha upasuaji ambacho kitasaidia kumtoa mtoto salama.
Hata hivyo waziri Ummy alizitaka hospitali za DDH na CDH ambazo zinamilikiwa na mashirika ya dini kufanya kazi kwa kuzingatia sera na miongozo ya afya na kufanya kazi kwa pamoja na Serikali kwani hospitali hizo zimeingia ubia na serikali hivyo watoe huduma kama inavyoelekezwa na serikali ikiwemo huduma bure kwa akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano pamoja na wzee wasio na uwezo
Kwa upande wa watumishi Waziri huyo alikiri Rukwa kuwa na idadi ndogo ya watumishi wa kada ya afya hivyo ameahidi katika kibali kijacho cha ajira atawapa kipaumbele “ila nawataka mtoe mahitaji sahihi ili tuweze kuondoa changamoto hizo, ila kwa sasa mnaweza kuwatawanya baadhi ya watumishi kwenye uhaba zaidi ili muweze kuongeza nguvu kwenye vituo vya kutolea huduma ili kuokoa maisha ya watanzania”
Waziri wa Afya aliwasihi watumishi wa sekta yake kuacha kufanya kazi kwa mazoea,wanatakiwa kujituma na kuwa waadilifu kwani mambo yamebadilika hivyo kuweka mifumo rahisi nay a kirafiki kwa wananchi ya kutoa malalamiko
“Wakuu wa Wilaya kama kuna Daktari ama Muuguzi amekosa tuleteeni watumishi hao tuwapeleke kwenye mabaraza ya kitaaluma ,na hivi sasa tumeanza kuwafutia leseni baadhui ya watumishi wa kada ya afya ambao hawatotimiza wajibu wao katika sehemu ya kazi

Reviewed by crispaseve
on
09:14
Rating:
Post a Comment