SHAKA AMALIZA ZIRA YA KIKZAZI PEMBA, AMTUMIA SALAMU MAALIM SEIF
Kaimu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndg Shaka Hamdu Shaka akiagana na
viongozi wa Chama Cha Mapinduzi mara baada ya kumaliza ziara ya siku nne
ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi Visiwani Pemba.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndg Shaka Hamdu Shaka akiagana na
viongozi wa Chama Cha Mapinduzi mara baada ya kumaliza ziara ya siku nne
ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi Visiwani Pemba.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndg Shaka Hamdu Shaka akiagana na
viongozi wa Chama Cha Mapinduzi mara baada ya kumaliza ziara ya siku nne
ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi Visiwani Pemba.
Na Mathias Canal, Pemba
Kaimu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndg Shaka Hamdu Shaka amehitimisha ziara
ya siku nne ya kikazi Kisiwani Pemba-Zanzibar kwa kuzuru katika Mikoa
yote miwili ya Kusini Pemba na Kaskazini Pemba na Wilaya zake zote za
Wete, Mkoani, Chakechake na Micheweni.
Katika
ziara hiyo pamoja na mambo mengi alikagua na kushiriki kufanya kazi za
kijamii ikiwa ni pamoja na kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM
2015-2020, kushiriki kuona shughuli mbali mbali za uzalishaji Mali
kupitia makundi ya vijana na kuwasaidia kwa kuwaunga mkono ili kuongeza
mtaji wa miradi yao.
Alitumia
ziara hiyo kuzungumza na makundi ya vijana kwa nyakati tofauti,
viongozi wa CCM, jumuiya za CCM Pamoja na kushiriki shughuli zingine
mbalimbali za kijamii, kiuchumi na kisiasa na kuwaasa kukaa maskani
pekee pasina kufanya kazi za uzalishaji mali jambo ambalo litapeleka
mbele maendeleo katika jamii.
Katika
maeneo yote aliyozuru Kaimu Katibu Mkuu huyo alitilia zaidi msisitizo
kwa vijana kujiunga na vikundi mbalimbali vya kijamii ili kupatiwa
mikopo ya vijana inayotolewa na serikali kwa asilimia 5 kila mwezi.
SALAMU KWA MALIM SEIF
Katika
hatua nyingine Shaka alimtumia salaamu Katibu Mkuu wa Chama Cha
Wananchi CUF aliyesimamishwa uongozi Maalim Seif Shariff Hamad kwa
kumtaka kuacha kueneza chuki kwa wananchi dhidi ya serikali yao kwani
kuhubiri siasa za mgawanyiko ni utaratibu wa kiongozi asiyekuwa mweledi
kwani maendeleo hayahitaji ubaguzi dhidi ya wananchi.
"Juhudi
za SMZ na SMT katika kuwatumikia wananchi hazitadumazwa kwa maneno ya
wapinzani badala yake zitaendeleza mikakati yake ya kutekeleza ilani ya
uchaguzi ya ccm ya mwaka" Alisema Shaka
Alisema
ni Siasa uchwara kuhubiri mgawanyiko katika jamii na kutumia nasaba na
asili ili kusaka madaraka, kiongozi ambaye atajiegemeza katika siasa
chafu milele hawezi kupata ridhaa ya wananchi.
"Nimeshiriki
ujenzi wa shina hili nikiwa na furaha kwenye mtima wangu, Msisahau
kumpelekea salamu Maalim Seif Shariff Hamad mwambieni asichoke kueneza
siasa za mgawanyiko CCM na serikali zake haizitaacha kabisa kuwapelekea
maendeleo wananchi bila kuwabagua" Alisema Shaka
Shaka
alisema kuwa Kiongozi au mwanasiasa anayekusudia kupata imani na amana
ya wananchi hawezi kushiriki kuwagawa watu bali huwa kiranja wa
kuwaunganisha na kuwataka wawe wamoja huku wakiishi kwa maelewano na
mshikamano.
Alisema
kuwa Wakati dunia, vyama vya siasa makini, wanaharakati na mashirika ya
kimataifa yakihubiri uwepo wa amani, maelewano na kukataa mgawanyiko,
itashangaza kumsikia mtu anayejiita kiongozi akihubiri siasa chafu za
mgaanyiko na mifarakano.
"Tunamsubiri
tena Seif Sharif Hamad mwaka 2020 tumpige mara ya saba, sijui atawania
Urais kwa CUF ipi, ile ya Profesa Lipumba haimtaki, yake yeye
haitambuliwi na Msajili wala hana Bodi ya Wadhamini, akija tutamgaragaza
ili aje kupumzika Mtambwe " Alisema Shaka
Ziara
ya Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndg Shaka Hamdu Shaka imeacha
gumzo kubwa kwa wananchi kufunguka kiakili na kumualika tena kwa mara
nyingine kwani tayari wamewelewa namna wanavyopotoshwa na viongozi wa
vyama vya upinzani.
SHAKA AMALIZA ZIRA YA KIKZAZI PEMBA, AMTUMIA SALAMU MAALIM SEIF
Reviewed by crispaseve
on
09:12
Rating:
Post a Comment