RC TABORA AIAGIZA KAMPUNI YA JOSSAM & CO LTD KUMALIZA BARABARA ZA KATA YA ULEDI NA ISEVYA KWA WAKATI ULIPANGWA.
Na Tiganya Vincent-RS –TABORA
SERIKALI
ya Mkoa wa Tabora imeiagiza Kampuni ya Jossam & co Ltd kuhakikisha
inakamilisha barabara ilizopewa za Uledi na Mwenge katika Manispaa ya
Tabora hadi kufikia mwishoni mwa Mwezi Septemba mwaka huu.
Agizo
hilo limetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri baada
ya kutembelea ujenzi wa barabara hizo zinazojengwa katika Kata ya Uledi
na Isevya ili kujionea maendeleo na kuhakikisha kama mjezni amezingatia
upana na urefu ullioandikwa katika makubaliano ya mkataba.
Alisema
kuwa kiasi cha shilingi milioni 700 zilizopangwa na Manispaa ya Tabora
kutumika kukamilisha mradi huo ni fedha nyingi ni vema Mkandarasi
anayejenga mradi huo akahakikisha anajenga katika kiwango bora na kwa
upana na urefu uliomo katika mkataba ili thamani ya pesa ionekane.
Mkuu
huyo wa Mkoa aliwaagiza Watendaji wa Wakala wa Barabara Vijijini na
Mijini (TARURA) kuhakikisha wanasimamia kwa karibu ujenzi wa barabara
hizo unazingatia matakwa yaliyoelezwa katika Mkataba wa Ujenzi ili
barabara hizo ziweze kutumika kwa muda mrefu bila kuharibika.
Awali
Mhandisi Msaidizi kutoka Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA)
Wilaya ya Tabora Stephen Warioba alisema kuwa ujenzi wa barabara hizo
unahusisha njia za waenda kwa miguu na ipaswa inamalize katika kipindi
kilichoelezwa katika Mkataba.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mwl. Queen Mlozi alimwakikishia Mkuu wa Mkoa
kuwa atafuatilia kwa karibu ili kuhakikisha kuwa kazi inayofanyika
katika eneo husika inazingatia mambo yote yaliyomo katika Mkataba na sio
nje ya hapo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Manispaa ya Tabora Bosco Ndunguru alisema kuwa baada ya
ujenzi wa Mradi huu kukamilika kutakuwepo na zoezi la upandaji wa miti
na maua kando kando ya barabara.
RC TABORA AIAGIZA KAMPUNI YA JOSSAM & CO LTD KUMALIZA BARABARA ZA KATA YA ULEDI NA ISEVYA KWA WAKATI ULIPANGWA.
Reviewed by crispaseve
on
09:09
Rating:
Post a Comment