TATIZO LA UMEME MTWARA NA LINDI KUPATIWA UFUMBUZI KATIKA KIPINJDI CHA SIKU 10: WAZIRI DKT.KALEMANI
Waziri
wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, akizungumza baada ya kutembelea kituo
cha kuzalisha umeme mkoani Mtawara leo Oktoba 16, 2017 ili kujionea kazi
inayofanywa na mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO)
kurekebisha mashine 8 kati ya tisa zilizoharibika. Kushoto ni Mkuu wa
Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, na kulia ni Kamu Mkurugenzi Mtendaji wa
TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka.
NA K-VIS BLOG/Mtwara.
Serikali
imewaomba wananchi wa mikoa ya Mtwara na Lindi kuwa na subira, katika
kipind hiki ambapo upatikanaji wa umeme kwenye mikoa hiyo umeathirika
baada ya mashine 5 kati ya 9 za kufua umeme (turbines) kuharibika.
Hata
hivyo Mafundui wa TANESCO wamekuwa katika juhudi kubwa za kuzifanyia
matengenezo mashine hizo, zilizofungwa miaka 10 iliyopita.
"tayari
tumeagiza vipuri kwa ajili ya kutengeneza mashine hizo ambazo kwa
ujumla wake huzalisha Megawati
18 za umeme, ambazo zitawasili ndani ya siku 7 ili kuweza kuondoa tatizo
la kuzimika umeme katika Mikoa ya Lindi na Mtwara." Alisema Dkt.
Kalemani.
Alisema,
baada ya kwasili kwa vipuri hivyo, kazi ya kuzifanyia matengenezo
itaendelea na amememuagiza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, kuleta
wataalamu wote wa TANESCO popote walipo nchini, wafika Mtwara na
kuungana na wataalamu waliopo ili kazi ya kuzitengeneza mashine hizo
iende kwa kasi.
Kati
ya mshine 9 ni mashine nne tu zinazotoa Megawati 8 ndio zinafanya kazi,
hali inayosababisha kuwepo kwa mgao wa umeme unaofikia hadi masaa 8 kwa
siku.
Dkt.
Kalemani ambaye amewasili mkoani Mtwara leo Oktoba 16, 2017 ili
kujionea juhudi za Mafundi wa TANESCO za kurejesha upatikanaji wa umeme
katika hali yake ya kawaida amesema vipuri hivyo vifungwe kwa muda wa
siku tatu badala ya wiki 3na kwamba ndani ya siku 10 umeme utakuwa
katika hali yake ya kawaida.
Mkoa wa Mtawara na Lindi unategemea mashine hizo zinazozalisha umeme unaotumia gesi asilia.
Ukiachilia
mbali kuharibika kwa mashine hizo, miundombinu mingine ya umeme kwenye
mikoa hiyo iko salama na katika ubora wa hali ya juu ambapo vituo vipya
vya kupoza na kusambaza umeme wa 132kV hapo hapo mkoani Mtwara na
kingine huko Mahumbika mkoani Lindi vinafanya kazi pamoja na ujenzi wa
njia ya kusafirisha umeme (transmission lines), nao uko katika hali
bora.
Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, (wapili kulia), Mkuu wa Wilaya ya
Mtwara, Mhe. Evod Mmanda, (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
TANESCO, Mhandisi Dkt,. Tito Mwinuka, wakitembelea kituo cha kufua umeme
mkoani Mtwara leo Oktoba 16, 2017.
Waziri wa Nishati Dkt. Medardi Kalemani, akizungumza
baada ya kutembelea kituo cha kuzalisha umeme mkoani Mtawara leo Oktoba
16, 2017 ili kujionea kazi inayofanywa na mafundi wa Shirika la Umeme
Tanzania, (TANESCO) kurekebisha mashine 8 kati ya tisa zilizoharibika
Fundi wa TANESCO, akitengeneza moja ya mashine zilizoharibika kwenye kituo cha kufua umeme mkoani Mtwara.
Fundi wa TANESCO, akitengeneza moja ya mashine zilizoharibika kwenye kituo cha kufua umeme mkoani Mtwara.
Fundi wa TANESCO, akichukua spana ili kuendelea na kazi.
Hii ni moja kati ya mashine zizlizoharibika.
TATIZO LA UMEME MTWARA NA LINDI KUPATIWA UFUMBUZI KATIKA KIPINJDI CHA SIKU 10: WAZIRI DKT.KALEMANI
Reviewed by crispaseve
on
07:45
Rating:
Post a Comment