Tanzania kuwakilishwa na timu mbili katika mashindano ya Cana kanda ya tatu ya kuogelea
Mchezaji wa kuogelea wa timu ya Taifa, Hilal Hemed Hilal akishindana wakati wa mashindano ya Taifa ya kuogelea.
Mchezaji wa kuogelea wa timu ya Taifa, Collins Saliboko akichuana katika mashindano ya Taifa ya kuogelea.
Dar es Salaam. Tanzania itawakilishwa na timu mbili za kuogelea
katika michezo ya kanda ya tatu ya kuogelaa ya Afrika yaliyopangwa
kuanza Alhamis katika bwawa la Hopac la jijini.
Tanzania imepewa nafasi ya kuwa na timu mbili kutokana na kuwa
mwenyeji.Katibu Mkuu wa Chama Cha kuogelea Tanzania (TSA) Ramadhan
Namkoveka alisema jana kuwa timu ya kwanza imepewa jina la Tanzanite
ambayo itakuwa na jumla ya wachezaji 30 na ya pili inajulikana kwa jina
la Platinum ambayo itakuwa na wachezaji 21.
Namkoveka alisema kuwa timu ya Tanzanite itakuwa na wachezaji 15
wanaume na 15 wanawake na ile ya Platinum itakuwa na wachezaji tisa
wanawake na 12 wavulana.Timu hizo zipo kambini hotel ya Giraffe chini ya
makocha, Alexander Mwaipasi na Michel Livingstone na zinafanya mazoezi
yake kwenye bwawa la Hopac kila siku.
Wachezaji wanaoumda timu ya Tanzanite ni Rania Karume , Chichi
Zengeni, Maia Tumiotto, Smriti Gokarn (Sonia Tumiotto, Anjani Taylor
ambao wote wanatoka klabu ya DSC, huku wengine ni Natalie Abwooli
Sanford (MIS), Anna Guild, Emma Imhoff (MSC), Sanne Kleinveld ( ISM
Moshi), Angelica Spence, Tara Behnsen, Tami Triller,Kayla Gouws na Amani
Doggart ambao wanatoka klabu ya Taliss.
Wachezaji wanaume ni Judah Miller, Elia Imhoff, Delvin Barick,
Caleb O’Sullivan, Khaleed Ladha na Matthew Guild wanatoka klabu ya
Mwanza, Chris Fitzpatrick (ISM Moshi), Marin DE Villard (DSC), Adil
Bharmal, Hilal Hilal, Harry McIntosh, Dhashrrad Magesvaran (Taliss) na
wanaotoka klabu ya shule ya kimataifa ya Morogoro ni Joseph Sumari,
Collins Saliboko na Dennis Mhini.
Wachezaji wanaounda klabu ya Platinum kwa upande wa wanawake ni
Shivan Bhatt, Natalia (Taliss), Charlotte Sanford, Vanessa Dickson
(MIS), Rebecca Guild, Meredith Boo (MSC), Maria Bachmann ( ISM Moshi),
Kayla Temba na Maya Somaiya ambao wote wanatoka klabu ya DSC.
Wanaounda timu ya wanaume ni Aravind Raghavendran, Mohameduwais
Abdullatif (Bluefins), Abraham Kayugwa( ISM Moshi), Terry Tarimo,
Aliasgar Chakera(Taliss), Zeke Boos (MSC), Yuki Omari, Augustino Lucas
(Champion Rise), Fallih Ahmed (Taliss), Carter Helsby (MSC), Ian
Lukaza(ISM) na Emmanuel Stenson wa shule ya kimataifa ya Morogoro.
Namkoveka alisema kuwa mchezaji Hilal Hilal ambaye yupo kambini
Dubai atajiunga na wenzake kesho katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa
na Vodacom Tanzania, Swissair, JCDecaux, Coca Cola, Label Promotions ,
Print Galore na Slipway Hotel.
Mbali ya Tanzania, mashindano hayo pia yatashirikisha waogeleaji kutoka nchi za Uganda, Rwanda, Sudan na Kenya.
Tanzania kuwakilishwa na timu mbili katika mashindano ya Cana kanda ya tatu ya kuogelea
Reviewed by crispaseve
on
07:46
Rating:
Post a Comment