RC SHIGELLA MGENI RASMI TANGA CITY MARATHON JUMAMOSI WIKI HII MJINI TANGA
Mratibu
wa Mashindano ya Riadha ya Tanga City Marathon, Juma Mwajasho kulia
akitetea jambo na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kuelekea
mashindano hayo Jumamosi wiki hiikushoto ni Meneja wa Mkwabi Super
Market ya Jijini Tanga ambao niwaandaaji wakuu wa mbio hizo,Kawkab
Hussein na Katibu wa Chama cha Riadha Mkoani Tanga (RT) Hassan Mwagomba
Katibu
wa Chama cha Riadhaa Mkoa wa Tanga (RT) Hassan Mwagomba akizungumza na
waandishi wa habari kuhusiana na uwepo wawashiriki kutoka Visiwa vya
Shelisheli, Unguja na Pemba ambao watapat afursa ya kuonyesha umahiri
wao kulia ni Meneja wa Mkwabi Super Marketya Jijini Tanga ambao ni
waandaaji wakuu wa mbio hizo,Kawkab Hussein,
Meneja wa Mkwabi Super Market ya Jijini Tanga ambao ni waandaaji wakuu wa mbio hizo, KawkabHussein akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano huu kuhusiana na zawadi zitakazotolewa msimu huu
Sehemu ya medali zitakazotolewa kwenye mashindano hayo
MKUU
wa mkoa wa Tanga, Martine Shigella ametarajiwa kushuhudia mashindano ya
riadha ya Tanga City Marathon msimu wa piliyanayotazamiwa kufanyika
Jumamosi wiki hii mjini hapa.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mratibu wa Mashindano hayo, Juma Mwajasho
alisema maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa huku baadhi ya
washiriki wakithibitisha kushiriki.
Alisema
katika mashindano hayo msimu huu watazamia washiriki zaidi ya600 ambapo
washindi watakabidhiwa zawadi mbalimbali zikiwemo medali ambazo
zimeandaliwa na wadhamini wa mashindano hayo.
Aidha
alisema mashindano hayo yatashirikisha wakimbaji kwenye umbali wa
kilomita 21,10 na 5 ambapo wataanzia mbio hizo kwenye eneo la Mkwabi
Super Market kuzunguka maeneo mbalimbali Jijini Tanga na kuishia eneo
hilo.
“Lakini kwa mara ya kwanza washiriki wote watakaoshiriki mashindano hayo watapewa medali na mgeni rasmi kwenye mashindano hayo.Kwa
upande wake, Katibu wa Chama cha Riadhaa Mkoa wa Tanga (RT) Hassan
Mwagomba alisema mashindano hayo pia yatashirikisha washiriki kutoka
Visiwa vya Shelisheli, Unguja na Pemba ambao watapata fursa yakuonyesha
umahiri wao.
Alisema
njia zitakazopitia mashindano hayo zimeboreshwa zaidi kiusalama kwa
wakimbiaji ili kuweza kuepukana na adhari zinazoweza kujitokeza wakati
yakiendelea.Naye
kwa upande wake,Meneja wa Mkwabi Super Market ya Jijini Tanga ambao ni
waandaaji wakuu wa mbio hizo,Kawkab Hussein alisema msimu huo
wameboresha mashindano hayo kwa kutoa zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi
wa kumi.
Alizitaja
zawadi zinazotolewa kuwa ni mshindi wa kwanza km 21 atapata700,000 wa
pili 500,000, huku mshindi wa tatu akipata 300,000 huku wengine kuanzia
wa nne hadi wa kumi watapata kifuta jasho cha 50,000.
Hata
hivyo alisema katika kilomita 10 mshindi wa kwanza atapata 250,000, wa
pili 150,000 na wa tatu 100,000 huku washindi wa kuanzia nafasi ya nne
mpaka 10 watapewa 30,000 pia kutakuwa na vituo maalumu kwaajili ya kutoa
huduma ya maji kwa wakimbiaji (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya
Tanga Raha)
RC SHIGELLA MGENI RASMI TANGA CITY MARATHON JUMAMOSI WIKI HII MJINI TANGA
Reviewed by crispaseve
on
10:49
Rating:
Post a Comment