Header AD

MKOA WA DAR ES SALAAM KUTOA CHANJO YA KUZUIA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI KWA WATOTO WA KIKE WA MIAKA 14


Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MAFUNZO ya utoaji wa chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi (Human vaccine) yametolewa leo jijini Dar es salaam na kuwataka watu wa kada zote kuhimiza watoto kupata kinga hiyo ya saratani.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameeleza kuwa chanjo hii itapunguza vifo vya wanawake wengi na ametoa rai kuwa kila mtoto wa miaka 14 apate chanjo hii na aturudie ili kukamilisha dozi kwa zoezi litakaloanza tarehe 23 mwezi huu.

Aidha amewataka wananchi kutumia fursa hii ya Serikali ya awamu ya tano kwa kujitokeza katika vituo 270 vilivyoorodheshwa na amewataka Wenyeviti wa Mitaa kuhamasisha akina Mama kupeleka watoto wao wakapate chanjo hii ili kuokoa maisha ya wanawake wengi pia ameeleza kuwa wana mpango wa kuendesha zoezi la kupima tezi dume nyumba kwa nyumba katika Mkoa wa Dar es salaam.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala bi. Sophia Mjema ameeleza kuwa kila mtoto wa miaka 14 apate chanjo hii na amewaomba akina baba kuwakumbusha akina Mama kuhusiana na chanjo hii.

Mratibu wa huduma za chanjo na uzazi Mkoa Bi. Ziada Sella ameeleza kuwa saratani ya shingo ya uzazi ni ya pili kwa madhara kwa mwanamke ikifuatiwa na saratani ya matiti ambayo huuwa wanawake wengi. Kuhusu dalili za awali la ugonjwa huo ameeleza kuwa kuvimba miguu, kutoka uchafu wa kahawia uliochanganyika na damu, maumivu ya miguu, mgongo na kiuno ni dalili za awali za saratani.

Kuhusiana na chanjo hii bi. Sella ameeleza kuwa watoto wa miaka 14 watapatiwa chanjo hii mara mbili kwa kurudia mara baada ya miezi 6 aidha watoto wenye maambukizi ya virusi ya Ukimwi (HIV) watapata chanjo tatu watakayorudia baada ya miezi 2 watakayochoma katika vituo vya afya na ya tatu watachoma na wenzao mashuleni baada ya miezi sita.

Aidha katika utoaji wa chanjo kuna vituo 270 ikiwa vituo 71 katika Manispaa ya Ilala, 48 Ubungo, 19 Kigamboni, 65 Kinondoni na 48 katika Manispaa ya Temeke.
Aidha amesisitiza wananchi kutokuwa na imani potofu kuhusu chanjo hizo kwani kinga ni bora kuliko tiba. Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda akizungumza leo katika uzinduziwa zowezi la utoaji Chanjo ya kuzuia Saratani ya mlango wa Kizazi.(Picha na Emmanuele Massaka,Globu ya jamii. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda akiteta jambo na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, kabla ya uzinguzi wa zowezi la utoaji Chanjo ya kuzuia Salatani ya mlango wa Kizazi.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt. Grace Maghembe akifafanua kuhusu zowezi la utoaji Chanjo ya kuzuia Saratani ya mlango wa Kizazi.
MKOA WA DAR ES SALAAM KUTOA CHANJO YA KUZUIA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI KWA WATOTO WA KIKE WA MIAKA 14 MKOA WA DAR ES SALAAM KUTOA CHANJO YA KUZUIA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI KWA WATOTO WA KIKE WA MIAKA 14 Reviewed by crispaseve on 10:14 Rating: 5

No comments

Post AD