BREAKING NEWS: LEMA ASHINDA RUFAA YAKE NA SASA KUENDELEA NA UBUNGE KAMA AWALI
Godbless Lema ambaye ni mbunge wa
Jimbo la Arusha Akiongea na wafuasi wa Chadema na baadhi ya wananchi
waliojitokeza kusikiliza hukumu ya kesi yake mara baada ya kushinda
rufaa yake leo katika Mahamaka Kuu
..............................................
..............................................
Taarifa zilizotufikia hivi punde
zinasema kuwa Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema
ameshinda rufaa yake ambayo ilikua inasikilizwa leo katika Mahakama Kuu.
Ambapo Kesi ya kupinga ubunge wake ilifunguliwa na makada wa tatu wa
CCM ambapo awali waliweza kumvua ubunge Lema Kwa Kushinda Kesi hiyo
iliyotolewa Hukumu katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha. Baadae Lema
alikata Rufaa kupitia kwa wakili wake Tundu Lisu huku wakiokatiwa rufaa
wakiwa na wakili wao Alute ambaye ni kaka yake Tundu Lisu.
Rufaa hii imechukua sura mpya
baada ya Wakili wa Upande wa Utetezi Ambaye ni Mh Tundu Lisu akiwa ni
mdogo wa damu kwa Wakili wa Waliokatiwa Rufaa Mh Alute, Hapa Ndipo
palipovuta hisia za watu wengi ukizingatiwa ilikua kama Mechi kati ya
CCM na Chadema huku Kaka na Mdogo Wake Wakipambana Vikali....
Taarifa Zaidi Zitawajia hapa hapa Lukaza Blog.
Reviewed by crispaseve
on
05:13
Rating:
Post a Comment