LINEX ACHOSHWA NA MASWALI ANAYOULIZWA KUHUSU JACKIE CLIFF.
Linex
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, Linex Sunday anayetamba na ngoma ya kamugina amejikuta akipitia katika kipindi kigumu kufuatia mashabiki na watu mbalimbali kumuulizia habari za model Jackie Cliff kukamatwa na sembe (madawa ya kulevya) Macau, China.
Kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, Linex aliona awachane Live wale wote wanaodhani kwamba alikuwa na ukaribu nae kiasi cha kuweza kujua mambo yake kisha kuwataka wasimsumbue kumuuliza taarifa zake kwani tangu alipofanya nae video hawakuwa na mawasiliano tena..
Hiki ndicho alichoandika Linex, kweli usupastaa kazi..
LINEX ACHOSHWA NA MASWALI ANAYOULIZWA KUHUSU JACKIE CLIFF.
Reviewed by crispaseve
on
21:07
Rating:

Post a Comment