RAPA DOE B WA GRAND HUSTLE AFARIKI DUNIA KWA KUPIGWA RISASI.

Rapa Doe B kulia akiwa na Rapa T.I wanaounda kundi la Grand Hustle.
Habari za kusikitisha zilizoenea katika mitandao mbalimbali Duniani kufuatia kifo cha rapa mchanga anayetokea katika kundi la Grand Hustle, ‘Doe B’(22) kufariki dunia baada ya kupigwa risasi katika klabu ya usiku iliyopo Montgomery, Alabama japokuwa sababu za kifo hazijaweza kujulikana bado.
Rais wa kundi la Hustle Grand, Rapa T.I kutoka ATL aliweza kutuma salamu za pole kwa mashabiki na familia ya marehemu kufuatia kifo hicho kupitia mtandao wa Instagram huku akionyesha kusikitishwa na taarifa alizozipata ukizingatiaRapa huyo mwenye umri mdogo alikuwa anakuja kwa kasi sana katika gemu ya muziki wa Hip Hop Duniani.
Doe B aliwahi kutamba na ngoma aliyofanya kama Solo inayokwenda kwa jina la ‘Bury Me In Gold na nyingine kali, hii sio mara ya kwanza kusikika matukio ya wasanii wakipoteza maisha huku vyanzo vya vifo hivyo vikihusishwa na uhasama wa makundi pamoja na mafanikio makubwa , T.I aliandika hivi..
RIP to my lil brother Doe B. We gon miss u my nigga. U’ll never be forgotten & U WILL NOT DIE IN VAIN. We Love U champ. Always. Just rest now my nigga….WE GOT IT
RIP Doe B.
RAPA DOE B WA GRAND HUSTLE AFARIKI DUNIA KWA KUPIGWA RISASI.
Reviewed by crispaseve
on
21:10
Rating:

Post a Comment