Header AD

SOMA MKASA HUU WA KWELI UNAOSISIMUA NA KUTISHA ILA WENYE MAFUNZO YA KUTOSHA KWETU SISI.

buried 
Katika kijiji cha Matare wilaya ya Magumu Serengeti alikuwa akiishi bwana mmoja aliyeitwa  Wambura,  siku moja isiyo na jina alishangaa ghafla akiwa mikononi mwa polisi kwa kesi ya kusingiziwa kisha kuhukumiwa kwenda jela miaka mitatu.
 Huku nyuma akiacha mke na watoto wanne waliokuwa wanasoma. Hukumu hiyo ilimtesa sana kichwa chake,  alitamani kila mtu anayemhisi anamakosa aingie katika moyo wake na kuupata ukweli.  Alilia sana na umaskini wake,  labda angepata wakili mzuri angeweza kumtetea,  kitendo chake cha kumkosa wakili kukahalalisha kifungo hicho.
 Alikwenda gerezani huku akiumia sana rohoni. Alianza maisha mapya kwa shida sana,  akawa mnyonge kila wakati na mwili wake ukapoteza afya kwa ujumla,  huko gerezani alifanikiwa kupata rafiki aliyekuwa na cheocha ama jukumu la uzikaji wa wafungwa hasahasa ambao hawakuwa na ndugu ama ambao ndugu zao huwa hawajitokezi pale gerezani.
 Rafiki wake mpya huyo ambaye alikuwa mzkaji alijaribu sana kumtia moyo Wambura na kumwaminisha kuwa hiyo ilikuwa hatua tu ya maisha ivyo anapaswa kukubaliana na hali halisi kwani ipo siku ukweli utakuja kujulikana. . Bwana Wambura yale maneno ya mzikaji hayakumuingia kabisa  alizidi kunyong’onyea.  ‘’Siwezi kuvumilia kukaa gerezani kwa miaka mitatu… kama unajali kilio change nisaidie nitoroke kwa namna yoyote ile ndugu yangu’’. Wambura alimsihi mzikaji.
 Siku moja mzikaji akamwambia bwana Wambura kuwa msaada umepatikana. Lakini yataka moyo,  ‘’Nipo tayari kwa lolte ili mradi tu nitoke humu ‘’ alijibu bila kumung’unya huku akimtegea sikio mzikaji .  ‘’Msaada pekee wa kukutorosha humu ndani ni kwa njia ya jeneza.  Yaani mfungwa akifa mimi nakuunganisha naye kwenye jeneza ‘’ .  akashusha pumzi kisha akaendelea ‘’wewe ukisikia kengele ya msiba njoo mara moja kwenye chumba cha maiti utakuta tayari sanduku liko katikati ya chumba linakuwa halijafungwa,  funua mfuniko ingia ndaniyake ulale pembeni ya maiti kwani sanduku huwa kubwa la kutosha kila aina ya maiti na hata miili miwili inaingia,  kisha nitakuja kulipigilia misumari .  Baada ya muda tutalipakia kwenye gari na kutoka kwenda nje ya gereza makuburini nikiongozana na baadhi ya wafungwa na maaskari magereza.
Tutakuzika huko lakini baada ya dakika 20 hadi 30 nitarudi kukufukua. Hautaweza kushindwa kupumua kwa dakika hizo,  utatoka ukiwa huru’’ .
 Japokuwa wazo lilikuwa zuri lakini lilimtisha sana Wambura.  Hata hivyo akaona afadhali afanye hivyo kuliko kukaa gerezani miaka mitatu bila kosa. Siku moja akasikia kengele ya msiba,  akafanya kama alivyoelekezwa na mzikaji.  Akaenda kuingia chumba cha maiti,  kweli alikuta sanduku huku akiwa na hofu akaingia na kulala pembeni ya maiti iliyokuwepo,  mara akasikia mtu ameingia na kulipigilia msumari sanduku muda mfupi baadae sanduku likainuliwa na kuwekwa kwenye gari.
 Gari likatoka nje ya gereza hadi makaburini,  sanduku likashushwa na kuwekwa kaburini na kuanza kufukiwa,  Wambura alijitaidi sana kuvumilia japo hofu ilizidi kumtanda,  ALIMTEGEMEA SANA MZIKAJI na alianza kumuona mkombozi wa maisha yake  kama alivyoambiwa,  akasubiri dakika kumi,  ishirini.. zikapita kimya,  Dakika 30 kimya… Joto nalo likazidi kuongezeka.  “Nitavumilia hadi afike’’ alijisemea kisha akaongezea kauli ya ujasiri ‘’Kama nilitakiwa kuishi miaka mitatu kivipi dakika kadhaa za hapa kaburini zinishinde” kwa kuwa alishakaa kwenye jeneza kwa muda kiasi akatamani kujua aliyekufa ni nani.. ni kweli aliogopa kuitazama maiti lakini aliona kama inatisha zaidi ikiwa imefunikwa vile kuliko ikiwa wazi.
 Akaifunua upande wa usoni kwa kuwa kulikuwa na giza  nene alikodoa sana macho kuitazama.  Lahaula macho yakakutana na sura ya mzikaji alikuwa amekufa na amezikwa na ahadi zake za ukombozi.
 FUNZO : Usimtegemee  sana mwanadamu katika maisha yako,  kwanza ni dhambi,  pili mwanadamu anakumbana na vikwanzo kama unavyokumbana navyo wewe  hadi kumwendea yeye.
 Hivyo kumpatia maisha yako ni kuzidi kuyaweka rehani na hatarini zaidi,  kama umeonewa,  umesingiziwa,  unanyanyaswa.. mwachie Mwenyezi MUNGU afanye maamuzi.

 Haya mzikaji aliyetegemea atamfukua naye ni maiti,  tazama mateso atakayoyapata hadi kufa kwake. Bila shaka atatamani kurudi gerezani kwa miaka mingine kumi lakini haitawezekana tena.
SOMA MKASA HUU WA KWELI UNAOSISIMUA NA KUTISHA ILA WENYE MAFUNZO YA KUTOSHA KWETU SISI. SOMA MKASA HUU WA KWELI UNAOSISIMUA NA KUTISHA ILA WENYE MAFUNZO YA KUTOSHA KWETU SISI. Reviewed by crispaseve on 12:57 Rating: 5

No comments

Post AD