Header AD

WATU 13 WAFARIKI KATIKA AJALI ISUNA, SINGIDA




Hali ilivyokuwa baada ya ajali hiyo.
Habari zilizotufikia sasa hivi kutoka Singida zinasema watu 13 wamefariki dunia baada ya kutokea ajali ya magari mawili kugongana uso kwa uso eneo la Isuna mkoani humo.
Habari zinasema ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Toyota Noah na lori ambayo namba zake za usajili hazikupatikana mara moja. Watu 13 waliofariki walikuwa katika Noah iliyokuwa ikitokea Itigi na maiti zao zimehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida. 
Baada ya ajali hiyo, dereva wa lori na msaidizi wake walitokomea kusikojulikana.

Picha na Habari : Global Publishers.
WATU 13 WAFARIKI KATIKA AJALI ISUNA, SINGIDA WATU 13 WAFARIKI KATIKA AJALI ISUNA, SINGIDA Reviewed by crispaseve on 12:57 Rating: 5

No comments

Post AD