JK AWAAPISHA MAWAZIRI, MANAIBU MAWAZIRI WAPYA
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mawaziri wapya na wa zamani baada ya baadhi yao kuwaapisha Ikulu, Dar es Salaam leo. Pia katika picha hiyo wamo Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilali (wa nne kushoto msitari wa mbele), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (wa tatu kulia msitari wa mbele) na Katibu Mkuu Kiongozi. Ombeni Sefue (wa tatu kushoto msitari wa mbele).(PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
Waziri mpya wa Sheria na Katiba, Dk. Asha Rose Migiro (kushoto) akipongezwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda pamoja na mawaziri wengine baada ya kuapishwa na Rfais Jakaya Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akipongezwa baada ya kuapishwa
Mawaziri wapya walioapishwa wakipongezwa
Rais Jakaya Kikwete (kulia) akizungumza na Aza mtoto wa Naibu Waziri mpya wa Utalii na Maliasili, Mahamoud Mgimwa (kushoto)
Wairi mpya wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akiangalia wakati Rais Jakaya Kikwete akitia saini kiapo chake cha utii. Kabla Seif alikuwa Naibu waziri wa wizara hiyo.
JK akimkabidhi zana za kazi Waziri mpya wa Fedha, Saada Mkuya Salumu
JK akimkabidhi zana za kazi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Charles Kitwanga.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kulia) akiangalia wakati JK akitia saini kiapo chake cha utii
Nabu Waziri mpya wa Habari na Mafunzo ya Ufundi, Jenista Mhagama akila kiapo
Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi (kulia) akiangaia wakati JK akitia saini kiapo chake
Mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Mkamia akila kiapo cha kuwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
JK akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Majembe Auction Mart, sETH Mwamoto katika hafla ya kuwaapisha mawaziri na manaibu mawaziri wapya.
Waziri mpya wa Mambo ya Ndani, Chikawe akipongezwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP,Ernest Mangu wakati wa hafla hiyo.
JK AWAAPISHA MAWAZIRI, MANAIBU MAWAZIRI WAPYA
Reviewed by crispaseve
on
12:34
Rating:

Post a Comment