HOSPITALI YA RUFAA IRINGA YAPATIWA VIFAA
Meneja
wa kituo cha Redio Nuru Fm, Victor Chakudika cha mkoani Iringa
akimkabidhi Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya mkoa wa Iringa Rustica
Tung'ombe moja ya viti vinavyotumiwa na walemavu , makabidhiano hayo
yalifanyika katika hospitali hiyo mwishoni mwa wiki.'
baadhi
ya viti vya walemavu na fimbo za kutembelea vilivyotolewa na redio
Nuru Fm ya mkoani Iringa kwa hospitali ya rufaa mkoa wa Iringa(picha na
Denis Mlowe).
Baadhi ya Wafanyakazi wa Nuru FM wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Iringa
========= ======= ==========
HOSPITALI YA RUFAA IRINGA YAPATIWA VIFAA
Na Denis Mlowe,Iringa
SHIRIKA
lisilo la Kiserikali la Iringa Development of Youth Disabled and
Children care (IDYDC) kwa kushirikiana na Redio Nuru Fm ya mjini Iringa
wametoa misaada ya viti 5 vya kubebea wagonjwa na fimbo 20 za kutembelea
kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa vyote vikiwa na thamani ya
shilingi milioni 3.5
Sambamba
na kuisadia hospitali hiyo radio hiyo ilivisaidia vituo vya watoto ya
yatima vilivyoko mkoani hapa vya Huruma Center,Sabasaba Center na kituo
cha wazee Iringa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula, vifaa vya usafi,
sabuni na mipira kwa watoto hao.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi msaada huo wakati wakitimiza miaka mitatu tangu
kuanzishwa kwa kituo hicho, meneja wa radio Victor Chakudika,aliitaka
jamii kuwa na moyo wa kujitolea kwa jamii inayoishi katika mazingira
magumu kwa lengo la kuisaidia serikali majukumu ambayo wadau wenye
uwezo wanaweza kuyatatua.
Alisema
lengo la redio kuwa jirani na jamii inayowahudumia katika kuwapatia
matangazo yao ya kila siku hivyo misaada iliyotolewa ni kurudisha faida
kwa jamii hiyo na itakuwa inafanyika kila mwaka kwa kutoa misaada kwa
wanaohitaji hasa kwa wanaoishi katika mazingira magumu na vituo
mbalimbli vya afya vilivyoko mkoani hapa.
Chakudika
alisema radio hiyo inatambua umuhimu wa kuchangia huduma za afya, kwani
bila wananchi husika kutokuwa na afya njema ina maana hata maendeleo
hayatakuwepo hivyo ni wajibu wao kwa kusaidiana na serikali ya Tanzania
kuhakikisha sekta ya afya inafanya kazi ipasavyo na kuwahudumia watu
wote kwa usawa.
Kwa
upande wake Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali hiyo Rustica Tung’ombe kwa
niaba ya Mganga mkuu aliishukuru radio hiyo kwa kujali na kuthamini
maisha ya Watanzania, kwa kuamini kuwa mchango huo si tu ni kusaidia
shughuli za hospitali bali pia utasaidia kuongeza viti katika hospitali
hiyo na kuwasaidia wagonjwa walemavu katika kufanya mazoezi pindi
wanapohitaji huduma ya vifaa hivyo.
HOSPITALI YA RUFAA IRINGA YAPATIWA VIFAA
Reviewed by crispaseve
on
11:24
Rating:

Post a Comment