Serikali ya Tanzania kuendelea kuimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Waziri
wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta (katikati) akifafanua kwa
waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu Serikali
ya Tanzania ilivyodhamiria kuimarisha ushirikiano baina yake na nchi wanachama
wa Jumuiya hiyo. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Amantius
Msole na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi
Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa.
Waziri
wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta akiwaeleza waandishi wa habari
(hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam juu ya Shirikika la ndege la Tanzania (ATCL) kupanua
huduma zake na kufika Bujumbura nchini Burundi, ATCL ilianza kufanya safari
zake kati ya Tanzania na Burundi Desemba16, 2013 mara tatu kwa wiki kama moja
ya hatua za kuimarisha usafiri wa anga kati ya nchi wanachama. Kushoto ni Naibu
Katibu Mkuu Wizara hiyo Amantius Msole.
1 Waziri
wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta akisisitiza kwa waandishi wa
habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu Tanzania itakavyonufaika
na mfumo wa himaya moja ya forodha katika kuimarisha biashara kati ya nchi
wanachama wa Jumuiya hiyo.(Picha
zote na Frank Mvungi-Maelezo).
Serikali ya Tanzania kuendelea kuimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Reviewed by crispaseve
on
15:13
Rating:

Post a Comment