PICHA KUTOKA JESHI LA MAGEREZA NCHINI: KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MBARAK ABDULWAKIL AZINDUA RASMI "DUTY FREE SHOP" - GEREZA KUU RUANDA, JIJINI MBEYA

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akionesha jiwe la Msingi
kwa Wageni Waalikwa mbalimbali(hawapo pichani) waliofika kushuhudia
uzinduzi rasmi wa Magereza "Duty Free Shop" ya Gereza Kuu Ruanda, Jijini
Mbeya leo Februari 12, 2014(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza Nchini, John Casmir Minja(wa pili kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu
wa Military Transit Shops LTD, Afzal Meghji.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ndg. Mbarak
Abdulwakil(katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Magereza
"Duty Free Shop" ya Gereza Kuu Ruanda, Jijini Mbeya leo Februari 12,
2014(kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu wa Transit Military Shops LTD, Ndg.
Afzal Meghji(kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini,
John Casmir Minja ambapo hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Ofisi
za Magereza Mkoa wa Mbeya.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa
maelezo mafupi ya utangulizi juu ya Mpango unatekelezwa na Jeshi la
Magereza kwa mafanikio makubwa wa ujenzi wa Magereza "Duty Free Shops"
katika Mikoa mbalimbali hapa Nchini kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi
kuzindua rasmi duka hilo ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Ndg. Mbarak Abdulwakil(hayupo pichani).

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ndg. Mbarak Abdulwakil
akitoa hotuba fupi ya uzinduzi rasmi wa Magereza "Duty Free Shop ya
Gereza Kuu Ruanda, Jijini Mbeya leo Februari 12, 2014 katika Viwanja vya
Ofisi za Magereza Mkoa wa Mbeya.

Baadhi ya Wageni Waalikwa toka Ofisi mbalimbali za Taasisi za Serikali
na Binafsi wakisikiliza hotuba fupi ya Mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ndg. Mbarak Abdulwakil(hayupo
pichani). Hafla hiyo fupi ya uzinduzi wa Magereza "Duty Free Shop" ya
Gereza Kuu Ruanda, Mbeya imefanyika leo Februari 12, 2014 katika Viwanja
vya Ofisi za Magereza Mkoa wa Mbeya.

Muonekano wa bidhaa mbalimbali za majumbani ambazo zinapatikana katika
"Duty Free Shop" ya Gereza Kuu Ruanda, Mbeya ambalo limezinduliwa leo
Februari 12, 2014 na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mbarak Abdulwakil(hayupo pichani). Duka hilo litawanufaisha Maafisa na
Askari wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Mbeya pamoja na
familia zao.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ndg. Mbarak
Abdulwakil(kulia) akiangalia vinywaji vya aina mbalimbali
vinavyopatikana katika duka hilo kama vinavyoonekana baada ya kuzindua
rasmi Magereza Duty Free Shop ya Gereza Kuu Ruanda, Mbeya leo Februari
12, 2014 (kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini,
John Casmir Minja. Duka hilo itakuwa linawahudumia Maafisa na Askari wa
Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Mbeya pamoja na familia zao.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ndg. Mbarak Abdulwakil(wa
tatu toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya(waliosimama) mara baada ya kuzindua
rasmi duka hilo leo Februari 12, 2014 Gereza Kuu Ruanda, Jijini Mbeya(wa
tatu toka kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini,
John Casmir Minja(wa pili toka kulia) ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya
Mbeya, Mhe. Noel Petre Chocha(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Fedha na
Utawala, Gaston Sanga(wa kwanza kushoto) ni Mkrugenzi Mkuu wa Military
Transit Shop LTD, Ndg. Afzal Meghji(wa pili toka kushoto) ni Katibu
Tawala Mkoa wa Mbeya, Bi. Mariam Mtunguja.Picha zote na Lucas Mboje wa
Jeshi la Magereza
PICHA KUTOKA JESHI LA MAGEREZA NCHINI: KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MBARAK ABDULWAKIL AZINDUA RASMI "DUTY FREE SHOP" - GEREZA KUU RUANDA, JIJINI MBEYA
Reviewed by crispaseve
on
05:47
Rating:
Reviewed by crispaseve
on
05:47
Rating:

Post a Comment