BAO LA KAVUMBANGU DHIDI YA AZAM, LAKATISHA UHAI WA SHABIKI HUYU.
SHABIKI wa Timu ya Yanga SC,
Deodatus Isaya Lusinde, mkazi wa Kipunguni A, amefariki dunia leo baada
ya kuanguka ghafla wakati akishangilia bao la Yanga lililofungwa na
Didier Kavumbagu katika dakika ya 14 kipindi cha kwanza.
Marehemu amepoteza maisha
akiwa chumba cha matibabu mara baada ya kuwekewa mashine ya oksijeni na
taarifa kuhusu kifo cha shabiki huyo zimethibitishwa na mmoja wa
madaktari aliyemhudumia akiwa uwanjani kabla ya mauti kumfika, Nassor
Matuzya.
Bwana Isaya alikuwa Meneja
wa Bar ya Rose Hill iliyopo Segerea jijini Dar. Ameacha mke aitwaye,
Rose William Lusinde ambaye ni askari magereza.
Marehemu amekutwa na mauti
hayo wakati wa mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, kati ya timu yake ya
Yanga na Azam, mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.
Mungu ailaze roho ya mwanamichezo, Deodatus Isaya Lusinde mahali pema peponi. AMEN!
Habari na Shaffih Dauda
BAO LA KAVUMBANGU DHIDI YA AZAM, LAKATISHA UHAI WA SHABIKI HUYU.
Reviewed by crispaseve
on
13:43
Rating:

Post a Comment