Header AD

VAN PERSIE AIBEBA MAN UTD, YAFUZU ROBO FAINALI KWA KUITANDIKA OLYMPIAKOS 3-0, WAUNGANA NA DORTMUND.


Double up: Van Persie slots home from close range to make it 2-0 to United
STRAIKA wa kimataifa wa uholanzi, Rob Van Persie ameonyesha makali yake kwa kuifungia ‘Manchester United’ goli tatu ‘Hat Trik’ katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya na kuiwezesha kufuzu hatua ya robo fainali kwa ushindi wa bao 3 -0 dhidi ya Olympiakos ya ugiriki na kuwasahaulisha wapenzi wa timu hiyo kipigo cha bao 3 walichokipata kutoka kwa mahasimu wao, klabu ya Liverpool katika dimba la Old Trafford.
Ahead: Rooney stepped over the free-kick and left it for Van Persie, who wrong-footed Roberto
Huko nchini Ujerumani pamoja na Dortmund kufungwa nyumbani kwenye uwanja wa Signal Iduna Park mabao 2-1 na Zenit St Petersburg ya nchini Urusi,ilifanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya ligi ya mabingwa barani ulaya kwa jumla ya mabao 5-3.
mabao ya Zenit hapo jana usiku yalifungwa na mshambuliaji raia wa Brazil Hulk kwa shuti kali na lingine lilifungwa na Salomon Rondon wakati lile la Dortmund lilifungwa na kiungo mkongwe Sebastian Kehl.

Wachezaji wa Borrusia Dortmund wakishangilia bao lao.
VAN PERSIE AIBEBA MAN UTD, YAFUZU ROBO FAINALI KWA KUITANDIKA OLYMPIAKOS 3-0, WAUNGANA NA DORTMUND. VAN PERSIE AIBEBA MAN UTD, YAFUZU ROBO FAINALI KWA KUITANDIKA OLYMPIAKOS 3-0, WAUNGANA NA DORTMUND. Reviewed by crispaseve on 13:45 Rating: 5

No comments

Post AD