Header AD

MAKAMU WA RAIS, DKT. BILAL ,AIWAKILISHA, TANZANIA ,KATIKA SHEREHE ZA MAADHIMISHO, YA MIAKA 50 YA UHURU ,WA MALAWI ,

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiagana na Rais wa Malawi, Profesa Arthur Peter Mutharika, baada ya shughuli za maadhimisho ya Sherehe ya miaka 50 ya uhuru wa Malawi kukamilika katika uwanja wa Civo, jana Julai 06, 2014. Nyuma yake ni Mama Asha Bilal. Picha na OMR.
  Wa pili (kushoto) ni Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Rais wa Malawi Profesa Arthur Mutharika akifuatiwa na mkewe, Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mama Asha Bilal na viongozi wengine wakifuatilia sala maalum ya kuombea nchi ya Malawi wakati wa sherehe za miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo zilizofanyika jana Jumapili Julai 06, 2014 katika uwanja wa Civo jijini Lilongwe, Malawi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiongozana na Mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Malawi Saulos Klaus Chilima kukagua gwaride maalum la makaribisho kwa Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Tanzania baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Lilongwe kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Malawi zilizofanyika Jumapili tarehe Julai 06,  2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenyeji wake 
Makamu wa Rais wa Malawi, Saulos Klaus Chilima, wakifurahia ngoma za asili za Malawi, wakati wa mapokezi kwenye Uwanja wa Lilongwe, alipowasili kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Malawi zilizofanyika Jumapili tarehe Julai 06,  2014.
MAKAMU WA RAIS, DKT. BILAL ,AIWAKILISHA, TANZANIA ,KATIKA SHEREHE ZA MAADHIMISHO, YA MIAKA 50 YA UHURU ,WA MALAWI , MAKAMU WA RAIS, DKT. BILAL ,AIWAKILISHA, TANZANIA ,KATIKA SHEREHE ZA MAADHIMISHO, YA MIAKA 50 YA UHURU ,WA MALAWI , Reviewed by crispaseve on 08:31 Rating: 5

No comments

Post AD