MAELFU WAMZIKA MEYIWA AFRIKA KUSINI LEO
Maelfu ya watu wamehudhuria mazishi
ya aliyekuwa nahodha wa timu ya soka ya Afrika Kusini Senzo Meyiwa
yanayofanyika jijini Durban.
Meyiwa, mwenye umri wa miaka 27, alipigwa risasi Jumapili iliyopita,
baada ya majambazi kuingia nyumbani mwa mpenzi wake karibu na
Johannesburg.Mtuhumiwa wa mauaji ya Meyiwa alifikishwa mahakamani Ijumaa na alishitakiwa kwa mauaji dhidi ya mlinda mlango huyo maarufu nchini Afrika Kusini.
Kifo cha Meyiwa kilisababisha mshituko mkubwa nchini Afrika Kusini na yameonyesha kiwango cha juu cha uahlifu wa kutumia nguvu nchini humo.
Mazishi yanafanyika katika uwanja wa mpira wa miguu wa Moses Mabhida Stadium katika mji wa Durban nyumbani kwa Meyiwa.
Wengi wa waombolezaji wamevaa fulana zenye picha ya Meyiwa, mtu ambaye alikuwa kivutio kikubwa kimichezo.
Bendera nusu mlingoti
Rais Zuma ameamuru bendera ya taifa ipepee nusu mlingoti siku ya Jumamosi ili kumuenzi mlinda mlango huyo wa timu ya taifa.
PolisI wamesema Ijumaa kuwa mtuhumiwa wa mauaji ya Meyiwa alitambuliwa katika gwaride la utambuzi.
Mtuhumiwa huyo, Zanokuhle Mbatha, mwenye umri wa miaka 25, anakabiliwa na mashitaka ya mauaji na ujambazi wa kutumia silaha na anatarajiwa kufikishwa tena mbele ya mahakama Novemba 11.Polisi wametangaza zawadi kwa mtu atakayewezesha kupatikana kwa taarifa zaidi kuhusu shambulio hilo ili kuwanasa watuhumiwa wengine.
MAELFU WAMZIKA MEYIWA AFRIKA KUSINI LEO
Reviewed by crispaseve
on
09:28
Rating:

Post a Comment