WAZIRI WA AFYA MH. SEIF RASHIDI AZINDUA RASMI GHETTO RADIO KATIKA HOSIPITALI YA TEMEKE JIJINI DAR.
Waziri
wa Afya Mh. Seif Rashid akiongea na Wauguzi wa Hospitali teule ya Mkoa
wa Temeke, Wafanyakazi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm pamoja na wadau
mbalimbali wakati wa uzinduzi Rasmi wa Radio hiyo, ambayo lengo lake ni
kuwakomboa vijana wa Mtaani pamoja na vipindi vingine vya kuelimisha
Jamii na Burudani, Pia amewashukuru kwa kutoa msaada wa vifaa mbalimbali
ambavyo vitasaidia katika Hospitali hiyo leo Tarehe 1.11.2014
Mkurugenzi
wa Sibuka George Ndagali akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa
Ghetto Radio ya Sibuka Fm iliyo fanyika katika katika Hosipitali Teule
ya Mkoa wa Temeke Ambapo Ghetto Radio Imeweza kufunguliwa Rasmi Katika
Mkoa huo nakuweza kutoa Msaada Vifaa Mbalimbali pamoja na Madawa Ambavyo
Vyote kwa ujumla vimegharimu kiasi Cha Shilingi Milioni sita na Laki
sita.
Mkurugenzi
wa Ghetto Radio Matt Brouwer akizungumza neno wakati wa uzinduzi wa
Ghetto Radio ya Sibuka Fm Ambapo Bw.Brouwer Alisema kuwa Ghetto Radio
ilianzishwa nchini Kenya Miaka Sita iliyopita nakuweza kuwasaidia vijana
mbalimbali Hivyo wameweza kuingia Nchini Tanzania Ilikuendeleza kuwapa
vijana Fursa Na elimu INayo Tolewa na Kituo Hicho Kwa Hapa Nchini
Mganga
Mkuu wa Hospitali teule ya Mkoa wa Temeke Amaani K. Malima akitoa neno
la Shukurani kwa Timu nzima ya Ghetto Radio ya Sibuka Fm kwa kufanya
uzinduzi wa Radio yao katika Hospitali hiyo pia kutoa Msaada wa vitu
mbalimbali vitakavyo saidia katika eneo hilo.
Meneja
wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm Edward Lukaka akitoa maelezo machache
ya malengo ya Radio hiyo pia kueleza mikakati ya kuendelea kutoa msaada
wa vifaa mbalimbali vya tiba katika Vituo zaidi vya Afya.
Mkurugenzi
wa kituo cha afya cha Iran Nchini Tanzania Dkt. Farhad Arjomandi
akiwashukuru Ghetto Radio ya Sibuka FM kwa kuanzisha Kituo hicho pia na
wao wametoa vifaa vya matibabu kwa ajili ya kushiriki uzinduzi huo wa
Radio
Mwenyekiti wa Red Cross Mkoa wa Dar es salaam Leonard Masonu akitoa neno la Shukurani
WAZIRI WA AFYA MH. SEIF RASHIDI AZINDUA RASMI GHETTO RADIO KATIKA HOSIPITALI YA TEMEKE JIJINI DAR.
Reviewed by crispaseve
on
09:35
Rating:

Post a Comment